Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari wenzao kutoka Taa...
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari
wenzao kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini
Australia wakitoa huduma ya matibabu ya moyo bila ya kupasua kifua
(Catheterization) kwa mgonjwa. Kushoto ni Afisa Muuguzi Ayoub Mchau,
akifuatiwa na Dkt. Daniel Maclennan na Dkt. Peter Kisenge (kulia).
Afisa Muuguzi wa Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Ayoub Mchau akiendelea na maandalizi
ya kazi ya kutoa huduma ya matibabu ya moyo bila ya kupasua kifua
(Catheterization) kwa mgonjwa huku Dkt. Daniel Maclennan (kulia)
na Dkt. Peter Kisenge wakimtazama. Taasisi hiyo kwa
kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini
Australia hivi sasa iko katika kambi maalum ya siku sita ya upasuaji
kwa wagonjwa wa moyo na katika kambi hiyo wagonjwa 20 wanarajiwa kupata
matibabu.
Dkt. Bingwa wa Moyo kutoka
Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia akitoa
elimu kwa vitendo jinsi ya upasuaji wa moyo bila ya kupasua kifua
(Catheterization) kwa mgonjwa unavyofanyika. Taasisi hiyo kwa
kushirikiana na JKCI wako katika
kambi maalum ya siku 6 ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo ambapo kazi
hiyo inaenda sanjari na utoaji wa elimu kwa wataalamu wa ndani
wakiwemo madaktari, wauguzi, wagavi na mafundi wanaohusika na
utengenezaji wa mashine za kimatibabu.
COMMENTS