Mkurugenzi wa Mradi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mo...
Mkurugenzi
wa Mradi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), kutoka Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mohammed Milanga, akitoa taarifa
ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria kwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph
Nyamhanga (kushoto), alipokagua maendeleo ya mradi huo.
Meneja
Mradi wa BAM International ya Uholanzi, Erick Van Zuthem, akifafanua
jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kulia), alipokagua maendeleo
ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Mradi wa jengo
la tatu la abiria (Terminal III), kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Eng. Mohammed Milanga, alipokuwa akikagua mradi huo,
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Mradi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), kutoka Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mohammed Milanga, akitoa maelezo
ya maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo upande wa kushukia abiria kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto), alipokagua maendeleo ya mradi
huo.
Mafundi
wa umeme wakiendelea na kazi ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria
(Terminal III), jijini Dar es Salaam. Jengo hilo likikamilika litakuwa
na uwezo wa kuchukua ndege 21 kwa wakati mmoja na abiria milioni 6.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph
Nyamhanga, akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Mradi wa jengo la tatu la abiria (Terminal
III), kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mohammed
Milanga, alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria
(Terminal III), jijini Dar es Salaam.
(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano).



COMMENTS