Na Lulu Mussa- Songwe Wakazi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamehamasishwa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa Maji hayana mmad...
Na Lulu Mussa-Songwe
Wakazi
wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamehamasishwa kutunza Vyanzo vya Maji
kwakuwa Maji hayana mmadala wa kitu chochote. Waziri wa Nchi mwenye
dhamana ya Usimamizi wa Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba ameyasema hayo leo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua
mazingira nchini.
Akiwa
katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje, Waziri Makamba alishuhudia
uliochepushwaji wa Mto Kalembo kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, na
haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Aidha Waziri Makamba amemuagiza
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kuhakisha wanambaini
mtu/watu hao na kuwafisha katika vyombo vya Sheria.
Taarifa
iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ileje ilisema kwamba kumekuwa na
uvamizi katika Vyanzo vya Maji na Serikikali imeendelea na juhudi za
kuwaondoa kwa kuwapatia maeneo mengine ila baadhi ya wananchi hao
wamekuwa wakikaidi. Hali hiyo haikumfurahisha Waziri Makamba na kuagizia
kutumika mamlaka ya Dola. “Hatuwezi kuruhusu watu kuharibu Vyanzo vya
Maji na kuwabembeleza watoke” Makamba alilisitiza.
Waziri
Makamba amesema ni muhimu watu kutii Sheria na Mamlaka zilizopo,
ameagiza wakazi hao kupewa wiki mbili tu na baada ya hapo waondolewe kwa
nguvu kwani tayari maeneo mbadala kwa makazi yao yalisha ainishwa. Pia
Waziri Makamba ameahidi kutoa muongozo wa Sheria ndogondogo za Mazingira
za Vijiji na Vitongoji ili zitumike kama nyenzo za hifadhi ya Mazingira
Nchini.
Katika
hatua nyingine Waziri Makamba alitembelea Kijiji cha Lubanda, Kata ya
Lubanda na kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi na kuwasisitizia,
kutokokata miti ovyo, kutochoma misitu na kuepuka uchepushaji wa Vyanzo
vya Maji ikiwemo mito na Mabonde.
Pia
Waziri Makamba aliwashauri wakazi wa Lubanda kulima kilimo cha Matuta
ama makinga maji ili kuepuka mmomonyoko wa udongo katika miinuko. Aidha
Waziri Makamba ameunga mkono jitahada za wananchi wa Kata hiyo za ujenzi
wa Kituo cha afya kwa kuchangia bati Ishirini na nane (28). Waziri
Makamba anaendelea na ziara yake na leo amewasili katika Mkoa wa Rukwa.
Uharibifu
wa Mazingira unaofanywa na binadamu, pichani ni Mto Kalembo uliopo
katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje uliochepushwa kwa manufaa ya
baadhi ya mtu/watu, haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba
amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kutafuta
wahusika na kuwafikishwa kwenye Vyombo vya dola.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba akifafanua jambo kwa wananchi mara baada ya kuwapa fursa ya
kuuliza maswali katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya
Lubada Wilayani Ileje. Kushoto ni Bw. Stanford Kibona aliyeuliza swali.
COMMENTS