Serikali imewataka baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) walioshirikiana na wenzao wa Mamlak...
Serikali
imewataka baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
walioshirikiana na wenzao wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitisha makontena
zaidi ya 100 bila kukaguliwa na shirika hilo katika Bandari ya Dar es
Salaam kujisalimisha haraka.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw.Charles Mwijage alitoa agizo hilo
mwishoni mwa juma wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa Shirika
hilo.“Nimeanza kukusanya orodha ya majina ya watu waliosaidia kupitisha makontena haya na nikija nayo hawatapona,” alisema.
Aliwataka wote wanaojijua kuhusika kujisalimisha mapema na kutubu ili wasamehewe kabla haya hatua hiyo.Makontena hayo yalipitishwa katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni bila ya kuthibitishwa na shirika hilo.
Pia
aliitaka TRA kuacha kutoa makontena bila ya shirika hilo kuthibitisha
au kukagua ubora wa bidhaa zinazoingizwa hapa nchini sababu mwenye
mamlaka hiyo ni TBS.
Alisema
watakaotubu kuwa walishiriki waseme walishiriki vipi na lini,
walishirikiana na nani na wataje sehemu yalikopelekwa makontena hayo ili
serikali iweze kusaidia kukomesha hali hiyo.Alisema
anaamini kuwa waliofanya hivyo katika mamlaka hiyo walifanya kwa utashi
wao bila ya ushiriki wa viongozi wao na kwamba sasa wakati umefika wa
kukomesha tabia hiyo.
Alilitaka
baraza hilo kushirikiana na menejimenti na kuhakikisha matatizo
yanayojitokeza yanapatiwa ufumbuzi kwa maslahi ya nchi na kwamba
serikali itahakikisha inaongeza vitendea kazi na watumishi ili kufikia
malengo ya shirika.
Kwa
mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Egid Mubofu, baraza hilo
lina wajumbe 48 wanaotoka katika vitengo mbalimbali na litakaa kwa muda
wa miaka mitano.“Baraza
hili linaundwa kutokana na mkataba wa menejimenti na Chama cha
Wafanyakazi (RAAWU),” alisema Dkt. Mubofu na kuongeza kuwa menejimenti
itashirikiana na baraza kufanyakazi za shirika kwa tija.
Alisema wafanyakazi wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu katika majukumu yao ya kila siku.Mwenyekiti
wa bodi ya wakurugenzi (TBS), Prof. Mekanya Maboko alilitaka baraza
hilo kufanya kazi kwa kushirikiana na menejimenti na bodi kuhakikisha
shughuli za udhibiti wa ubora zinafanyika kwa ufanisi.
“Bodi itaendelea kuisimamia menejimenti na kuishauri ifanye kazi kwa kuzingatia sera na sheria,” alisema.
COMMENTS