Hawa ndio baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Malangali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ...
Hawa
ndio baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya
Malangali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika
shule hiyo na kukaangalia mazingira ya shule hiyo na kutafuta njia za
kutatua baadhi ya changamoto kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya
muungano ya Tanzania.
Mkurugenzi
wa
kampuni ya Yono Action Mart, Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la
Malangali Alumni Association (MAAS) akizungumza na wanafunzi wa
shule ya sekondari Malangali na kuwaeleza jinsi gani shule hiyo
ilivyowapa mafanikio hadi sasa walipofikia.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi
wa kampuni ya Yono Auction Mart, Yono Kevela ambaye ni mlezi wa Umoja wa
Malangali Alumni Association (MAAS), alisema kuwa maendeleo aliyoyapata sasa ni kutoka
na shule ya Malangali hivyo ameamua kurudi na kuisadia shule hiyo.
“Wafanyakazi na viongozi
mbalimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya shule tulizosoma ili
kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini Tanzania.” alisema Kevela.
Pia amesema kuwa shule
nyingi walizosoma viongozi, wafanya biashara na wajasiriamali mbalimbli
zinahitajika kukarabatiwa, hivyo amewataka wadau wote kuzikumbuka shule
walizosoma.
Naye Padre wa kanisa la Kikatoliki mkoani Mbeya Telesipholi Tweve aliwakata wanafunzi mbalimbali
waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio
chanzo cha mafanikio yao ya sasa.
“Leo nimerudi katika shule
hii ya Malangali kuja kusaidia kutatua changamoto ambazo zipo katika shule hii
ukizingatia kuwa shule hii inauchakavu wa majengo na miundombinu hivyo sisi
kama MAAS tumeanza kwa kukarabati ukumbi ambao utakuwa na faida kwao kwa
kutumia kwenye sherehe na kukodishwa pia”. alisema Tweve
Kwa upande wake mwenyekiti
wa Malangali Alumni Association (MAAS), Paul Mng’ong’o alisema kuwa wameanza
kuisaidia shule ya Malangali muda mrefu kwa kuwa tayari wameshakarabati ukumbi
wa shule, wamewanunulia Televisheni na King’amuzi kwa ajili ya habari na wanaendelea
kutatua matatizo ya shule hiyo.
“Hebu angalia sisi tuliosoma
hapa tumepata mafanikio lakini shule yetu bado ipo pale pale na inazidi
kuchakaa hivyo inatulazimu kuchangishana ili kurudisha fadhila kwa kuwa wengi
wetu tumepata mafanikio makubwa kwa kusomea kwenye shule hii, tuna viongozi wengi, wenye uwezo wengi, wakulima wakubwa sana hapa nchini wengi wamesoma katika shule
hii”, alisema Mng’ong’o
Lakini pia Mng’ong’o alisema
kuwa lengo la umoja wa MAAS ni kuunganisha wanafunzi wote
waliowahi kusoma shule hiyo kuweza kupeana mawazo ya maendeleo na
kusaidiana kufikia malengo.
Shule ya Malangali ni kati ya shule kongwe ambazo viongozi mbalimbali katika serikali, taasisi za umma na sekta binafsi walijengewa msingi wa awali wa maisha.
Katika mwaka wa bajeti huu serikali imetenga bajeti ya kukarabati shule kongwe zipatazo thelethini na saba (37) jambo ambalo wananfunzi hao wameomba serikali kuharakisha utekelezaji wake.
Shule ya Malangali ni kati ya shule kongwe ambazo viongozi mbalimbali katika serikali, taasisi za umma na sekta binafsi walijengewa msingi wa awali wa maisha.
Katika mwaka wa bajeti huu serikali imetenga bajeti ya kukarabati shule kongwe zipatazo thelethini na saba (37) jambo ambalo wananfunzi hao wameomba serikali kuharakisha utekelezaji wake.



COMMENTS