Marehemu Advocate Yusta Msoka enzi za uhai wake. Jumuiya ya wanafunzi kutoka Shule ya msingi Changa na Shule ya sekonda...
Marehemu Advocate Yusta Msoka enzi za uhai wake.
Jumuiya ya wanafunzi kutoka Shule ya msingi Changa na Shule ya sekondari Usagara zilizopo mkoani Tanga pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam tunasikitika kutangaza kifo cha aliyewahi kuwa mwanafunzi mwenzetu Marehemu Advocate Yusta Msoka kilichotokea Majuzi hapa Dar es salaam.
Sisi kama wanajumuiya wenzake kupitia shule mbalimbali tulizopitia tunatoa pole zetu kwa pacha mwenzake Mwanasheria Felista Msoka na wana familia kwa ujumla, tunaungana nao pamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Taarifa kutoka kwa familia ya marehemu zinasema mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho tarehe 17/10/2016 hapa jijini Dar es salaam katika makaburi ya Chamanzi - Mbagala ambako ni jirani na wazazi wake wanapoishi huko Mbagala kuanzia saa 5 asubuhi kwa kutanguliwa na Chakula/ Ibada kisha kuishiwa na Mazishi katika nyumba yake ya Milele.
Kwa wale wote ambao watapata taarifa hii tunaomba umjulishe na mwingine ili tuweze kuungana pamoja kumsindikiza mwenzetu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMIN.
COMMENTS