RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO VYA AJALI YA BASI LA BARCELONA
HomeJamii

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO VYA AJALI YA BASI LA BARCELONA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go...

WAZAZI MBURAHATI SACCOS YAIVA, KUPATA HATI YA USAJILI HIVI KARIBUNI
WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA
RAIS DKT. MAGUFULI AKIWA MAPUMZIKONI CHATO MKOANI GEITA








JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kufuatia vifo vya watu 11 vilivyosababishwa na ajali ya basi la kampuni ya Barcelona iliyotokea jana tarehe 17 Oktoba, 2016 katika eneo la Miteja Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Basi hilo lenye namba T 101 CUU lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kijiji cha Mahuta katika Wilaya ya Newala Mkoani Lindi, lilipinduka baada ya gurudumu lake la kushoto kupasuka na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo na mwingine 1 kufariki dunia baadaye akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Lindi, huku watu wengine 43 wakiwa wamejeruhiwa.
Katika salamu zake, Rais Magufuli amesema amepokea taarifa za vifo vya watu hao kwa mshituko na huzuni kwa kuwa kwa mara nyingine Taifa limepoteza watu wake na familia zimepoteza wapendwa wao na watu ambao ziliwapenda na kuwategemea.
"Ndugu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambia naomba unifikishie salamu nyingi za pole kwa wote waliopoteza jamaa na ndugu zao katika ajali hii, kwa hakika nimeguswa sana na vifo hivi na naungana na familia za marehemu wote katika maombolezo na sala" amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amewasihi wote walioguswa na vifo hivyo kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi na amewaombea Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Pia Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na kurejea katika shughuli za ujenzi wa Taifa,

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
18 Oktoba, 2016

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO VYA AJALI YA BASI LA BARCELONA
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO VYA AJALI YA BASI LA BARCELONA
https://lh6.googleusercontent.com/_yJimqLMF8Djsh3bWlbdeqMywQD_9ujf7iZcy63D7SriQM2AZbqVDAreCr59VMNkNz2Q6dAPOd2R1BY-x3TwRjYkxNy4hUCoQ5mgMmmIcQ4kYhgR-UeoHXSbMn1fCLNF8syXvC7h_qVrz1gIMQ
https://lh6.googleusercontent.com/_yJimqLMF8Djsh3bWlbdeqMywQD_9ujf7iZcy63D7SriQM2AZbqVDAreCr59VMNkNz2Q6dAPOd2R1BY-x3TwRjYkxNy4hUCoQ5mgMmmIcQ4kYhgR-UeoHXSbMn1fCLNF8syXvC7h_qVrz1gIMQ=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/10/rais-magufuli-atuma-salamu-za_18.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/rais-magufuli-atuma-salamu-za_18.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy