Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akiaga mwili wa Mw...
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Lilian Mapfa akiaga mwili wa Mwanasheria wa Wizara hiyo,
marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki wiki iliyopita na mwili wake
ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam jana. Nyuma ya Mapfa, ni Mkuu wa
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Wizara hiyo,
Jane Massawe.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba,
Afisa Sheria wa Wizara hiyo, Berious Nyasebwa wakiaga mwili wa
mwanasheria mwenzao wa Wizara hiyo, marehemu, Yusta Msoka, ambaye
alifariki wiki iliyopita na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es
Salaam jana.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Lilian
Mapfa (kushoto kwa Balozi), Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara
hiyo, Marlin Komba wakiwa katika hali ya huzuni pamoja na waombolezaji
wengine wakati wa kuaga mwili wa marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki
wiki iliyopita na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam
jana.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), tawi la
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi akisoma wasifu wa
Afisa Sheria wa Wizara hiyo, marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki
wiki iliyopita na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam
jana.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba,
akikabidhi rambirambi kwa niaba ya Ofisi ya Mwajiri wa Afisa Sheria,
marehemu Yusta Msoka. Kushoto anayepokea rambirambi hiyo ni Mama wa
marehemu huyo. Mtumishi huyo alifariki dunia wiki iliyopita na kuzikwa
jijini Dar es Salaam jana.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
COMMENTS