MKUU WA WILAYA YA HAI, BYAKANWA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KWA KUREJESHA SHAMBA LA FOFO ESTATE KWA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO
HomeJamii

MKUU WA WILAYA YA HAI, BYAKANWA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KWA KUREJESHA SHAMBA LA FOFO ESTATE KWA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO

Mkuu wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji vinne vilivyoko kata ya ...

RC MAKONDA APOKEA TANI 120 ZA SARUJI KUTOKA VYAMA VYA USHIRIKA 27 VYA MKOA WA DAR
MAKAMU WA RAIS KUONGOZA HARAMBEE UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA MACHI 16 DAR ES SALAAM
MASAUNI AZINDUA VITUO MWENDO SITA VYA POLISI, AWAASA WANANCHI KUJIKITA KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELE








Mkuu wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji vinne vilivyoko kata ya Machame Narumu akitoa uamuzi juu ya mgogoro wa ardhi wa shamba la Fofo Estate. 

Baadhi ya Wananchi waliofika katika Mkutano huo. 

Mkuu wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa (aliyenyoosha mikono) akitoa ufafanzi wa jambo mara baada ya kutangaza kurejesha eneo lenye mgogoro kwa Halmashauri ya wilaya ya Hai.

Baadhi ya wananchi wa vijiji vinne vya Urori,Tella, Mula na Usali waliohudhria mkutano wa Mkuu wa wilaya ya Hai wa kutoa maamuzi juu ya mggoro wa shamba la Fofo Estate. 


Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara na Mkuu wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa wakati akitoa uamuzi juu ya mgogoro wa Shamba hilo.
Shamba la Ekari 106 la Fofo Estate lililopo wilayani Hai ambao limekuwa na mgogoro kwa zaidi ya miaka 40. 


(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini).


MGOGORO wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 wa  shamba la Fofo lilipo wilayani Hai ,umemalizika baada ya Mkuu wa  wilaya hiyo, Gelasius Byakanwa kutangaza kurejesha shamba hilo chini ya usimamizi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai.


Hatua ya Mkuu huyo wa wilaya inatokana na mgogoro baina ya Wananchi wa vijiji vinne vya Urori,Tella, Mula na Usali vilivyoko kata ya Machame Narumu lilipo Shamba hilo dhidi ya aliyekuwa mtendaji mkuu wa Chama cha Ushirika cha Narumu Manushi,Peter Karanti anayedaiwa kujimilikisha shamba hilo .


Akitoa historia ya mgogoro huo Byakanwa alisema shamba hilo lililopewa namba 240 na 242 Ex .C.T No.NP 405 EP.LOT.661 (FOFO ESTATE) lilikuwa linamilikiwa na raia wa kigeni Dkt A Phones ambaye aliweka rehani shamba hilo mwaka 1966 kwa ajili ya mkopo wa kiasi cha Sh 100,000 kutoka benki ya CRDB .


“Baadae Dkt ,Phoneas alitoroka nchini kabla ya kulipa mkopo huo, Benki baada ya kugundua hilo ilichukua hatua ya kuliza shamba ili kurudisha mkopo aliokuwa akidaiwa Dkt Phoneas”alisema Byakanwa.


Alisema  Chama cha Ushirika cha Narumu Manushi ambacho wanachaa wake ni wananchi wa vijiji vine lilipo shamba hilo kilifanikiwa kununua shamba hilo kwa  kulipia deni la sh 100,000 ambapo kilitoa  kiasi cha Sh 20,000 huku kikibaki na deni la sh 80,000.


“Taarifa ambazo ofisi yangu ilizipata ni kuwa chama kilipewa miaka 10 kiwe kimemaliza kulipia deni hilo ,lakini ndani ya miaka miwili zikatokea taarifa za kuwa Chama cha Ushirika cha Narumu kilishindwa kumaliza deni lake”alisema Byakanwa.


“Bahati mbaya zaidi ,shahidi wa taarifa hizi ni Peter Karanti aliyekuwa mtendaji mkuu wa chama cha Ushirika na haikujulikana yeye kama mtendaji mkuu alichukua hatua gani za kuhakikisha chama kinamaliza deni lake”aliongeza Byakanwa.


Alisema hakuna ushahidi unaoonesha kuwa benki ya CRDB ilikususdia kuliuza shmaba hilo kwa kigezo cha kuwa Chama cha Ushieika cha Narumu kimeshindwa kulipa deni ndani ya muda husika zaidi ya kuwepo kwa taarifa kuwa Mtendaji mkuu wa Chama cha Ushirika alitafuta baadhi ya wanachama na wasio wanachama wachange pesa ya kulikomboa na kulimiliki.


“Baadae chama cha ushirika kilipitisha maamuzi ya kuwapa jukumu la kulipa deni la chama,Karanti na wenzake walilipa deni na kukabidhiwa Shamba hata hivyo walishindwa kupata hati miliki ya Shamba hilo kwa kuwa ilikua bado inashikiliwa na benki kutokana na mkataba uliokuwepo ulikuwa ni Chama cha Ushirika na si Karanti na wenzake.


Akitoa maamuzi juu ya mgogoro huo  wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji hivyo uliofanyika katika uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Tunoma ,Byakanwa alitangaza kuzuia kufanyika kwa shughuli za maendeleo katika shamba la Fofo zinazofanywa na mtu binafsi.


“Kwa kuwa hati ya Dkt Phoneas aliyekuwa mmiliki wa shamba hilo ilikwisha batilishwa na kuamuliwa shamba hilo limilikishwe kwa kijiji na vijiji ndivyo vinalipa kodi ya ardhi,wakulima wote waliolima katika shmba hilo wavune mazao yao ndani ya kipindi cha miezi mitatu” alisema Byakanwa.


Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati  ya ufuatiliaji wa shamba hilo John Kweka alisema awali Wenyeviti wa vijiji hivyo ndio walikuwa wakifuatilia mgogoro huo kabla ya kubaini kuwa wenyeviti hao kuwa na maslahi katika mgogoro na kulazimika kuunda kamati nyingine.


“Tumefuatilia hili suala hadi kwa Waziri wa Ardhi,tumepokea kwa furaha maamuzi  ya mkuu wetu wa wilaya kwa sababu sisi kama kamati tulipendekeza maeneo katika hili shamba yatumike kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati, Shule, Taasisi, Soko  na Mahali pa kuzikia hili ndio lilikuwa lengo letu”alisema Kweka.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKUU WA WILAYA YA HAI, BYAKANWA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KWA KUREJESHA SHAMBA LA FOFO ESTATE KWA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO
MKUU WA WILAYA YA HAI, BYAKANWA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KWA KUREJESHA SHAMBA LA FOFO ESTATE KWA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhWvDsbF-gIoxtgA15pC6CxqLVo2Fhe5xG4ZmV0_A4spuKktGJfNbzBsRrFImGM1k4_xQK2_HjvPIPN5TB3-ZadhXw6-TDLkWXcmzfhbmIl0ifuLJpP6MwU8QENdr26whYwaCP3YGZfnCdZ/s640/IMG_2947+%25281024x683%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhWvDsbF-gIoxtgA15pC6CxqLVo2Fhe5xG4ZmV0_A4spuKktGJfNbzBsRrFImGM1k4_xQK2_HjvPIPN5TB3-ZadhXw6-TDLkWXcmzfhbmIl0ifuLJpP6MwU8QENdr26whYwaCP3YGZfnCdZ/s72-c/IMG_2947+%25281024x683%2529.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/10/mkuu-wa-wilaya-ya-hai-byakanwa-amaliza.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/mkuu-wa-wilaya-ya-hai-byakanwa-amaliza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy