Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. MAENDELEO ya Viwanda yanahitaji mali ghafi za kilimo hivyo Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (T...
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MAENDELEO
ya Viwanda yanahitaji mali ghafi za kilimo hivyo Benki ya Maendeleo ya
Kilimo nchini (TADB) inawajibu ya kuwafikia wakulima ili matokeo ya
viwanda yaweze kuonekana ikiwemo na kuwa na masharti ya riba nafuu au
kuondolewa kabisa.
Hayo
ameyasema leo Naibu Waziri wa Fedha , Uchumi na Mipango, Dk. Ashantu
Kijaji wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo
(TADB), amesema kuwa sekta ya kilimo inaajiri watanzania asilimia 70
huku ikichangia pato la Taifa kwa asilimia 28 ambayo ni kidogo kutokana
na ukuaji wa sekta ambayo inatakiwa kwenda na viwanda ambapo TADB ndio
yenye kuweza kuleta mapinduzi hayo viwanda kwa kuwafikia watanzania
waliowengi.
Amesema
bodi ya wakurugenzi ya TADB inajukumu la kutekeleza na kuboresha sekta
ya kilimo kwa kuwafikia watanzania wengi katika maeneo ya kijijini
kutokana ni kuwa wazalishaji wa mazao mbalilmbali ambayo ndio yanaweza
kuzalisha viwanda na nchi ikaweza kukua kiuchumi pamoja na kuongeza pato
la taifa.
Dk.
Ashantu amesema benki ya kilimo ihakikishe wanatafuta vyanzo vya fedha
ili waweze kukuza mtaji na kutoa mikopo kwa wakulima kwa masharti nafuu
katika kumfanya mkulima kuweza kunufaika kilimo chake.
"TADB
ina deni kubwa kwa wakulima sasa ni wakati umefika wa bodi kufanya kazi
kwa uadilifu katika kuinua sekta ya kilimo kwa kutoa mikopo na sio kwa
bodi kufanya mikutano nje ya nchi na kuacha kutatua changamoto ya mikopo
katika sekta hiyo" amesema Dk. Ashantu.
Nae
Mweenyekiti wa Bodi hiyo, Rosebudy Kurwijla ameiomba serikali
kuiwezesha benki ili kuweza kufikia wananchi waliowengi na wanahitaji ya
kukopeshwa na TADB katika kuendeleza kilimo.
Amesema kilio cha TADB ni mtaji na bila kufanya hivyo itakuwa ni vigumu kuwafikia wananchi waliowengi.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Thomas Samkyi amesema mpango
wao ni kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Maendeleo
ya Afrika katika kuweza kupata mtaji wa kuweza kuwakopesha wakulima
ili kuweza kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya
Viwanda.
Mwenyekiti
wa Bodi wa TADB, Rosebudy Kurwijila akizungumza katika uzinduzi juu ya
majukumu ya bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Fedha, Uchumi na Mpango, Ashantu Kijaji akizungumza wakati
uzinduzi wa Bodi ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) leo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Ashantu Kijaji akipokea mfano wa
hundi ya Sh.milioni tano kwa ajili ya tetemeko la Ardhi mkoani Kagera
leo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Fedha, Uchumi na Mpango, Dk.Ashantu Kijaji akiwa katika picha
ya pamoja na wajumbe wa bodi wa TADB leo jijini Dar es Salaam.
COMMENTS