GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA WATOA ELIMU JUU YA KUDUMISHA AMANI KATIKA FAMILIA, JUKWAA LA VIJANA JIJINI DAR
HomeJamii

GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA WATOA ELIMU JUU YA KUDUMISHA AMANI KATIKA FAMILIA, JUKWAA LA VIJANA JIJINI DAR

Kila Baada ya Mwezi kikundi cha Tandale Youth Development Centre hufanya Jukwaa la Vijana ambapo vijana hukutana na kujadili mambo mbali...

UFUNGUZI WARSHA YA MAAFISA HABARI ATAWAS
MAELEZO TV :SERIKALI KUANZA KUTOA ELIMU YA MLIPA KODI MASHULENI
WAZIRI MKUCHIKA ATETA NA BALOZI WA USWISS



Kila Baada ya Mwezi kikundi cha Tandale Youth Development Centre hufanya Jukwaa la Vijana ambapo vijana hukutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na wao. Katika jukwaa la mwezi huu kulikuwa na mada inayosema: "Nafasi  ya mtoto wa kike katika jamii" ambapo majadiliano yalilenga zaidi kutambua nafasi hizo, changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike pamoja, namna ya kuzitatua na jinsi gani mtoto wa kike anavyoweza kusimamia malengo yake kufanikiwa.

Aidha katika jukwaa hilo la vijana Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation  kupitia Mkurugenzi Mkazi wa hapa nchini, Martha Nghambi alitoa pia elimu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha  amani ndani ya familia, ambapo alisema kuwa ili amani iweze kudumishwa na watu waishi bila kuwepo na mifarakano ni lazima kujenga mahusiano mazuri kuanzia chini yaani wanafamilia kuweza kuelewena kwa kuwahusisha wazazi na watoto ambapo hawa wakiishi vema basi hakutakuwa tena na uvunjifu wa amani na kusisitiza kuwa kila mtu analojukumu la kulinda amani.
Mwendeshaji wa Jukwaa la Vijana lililofanyika Tandale leo Jamal Magabilo akitoa neno la utangulizi na kuwakaribisha wageni waalikwa wote katika jukwaa.
Mkurugenzi wa Gida Rahma Bendera akiitambulisha rasmi mada katika Jukwaa la vijana inayosema nafasi ya mtoto wa kike katika jamii.

Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi akitoa Elimu kwa kina juu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha amani kwenye familia ambapo aligusia mambo mengi ikiwa ni pamoja na visababishi vya uvunjishi wa amani pamoja na namna ya kuzuia uvunjifu huo wa amani katika familia.

Mwandaaji wa Matukio wa TYDC Imani akitoa neno la shukurani kwa wote waliohudhulia jukwaa hilo.

Afisa Mahusiano wa TYDC Anna Emmanuel akielezea historia fupi ya umoja wao.

Mdahalo ukiwa umeanza.

Loveness Msuya akizungumzia mada inayohusu jinsi gani mtoto wa kike anaweza kusimama kwenye ndoto na malengo yake na mwisho wasiku kufanikiwa, alieleza njia na mbinu mbalimbali zinazoweza kumfikisha mtoto wa kike kule anapo pataka.
Anna Mwalongo kutoka DUCE akisisitiza kwa nguvu na kupaza sauti ya kuwasihi Mabinti kujitambua ili waweze kuepukana na vishawishi mbalimbali vinavyo sababishwa na vijana.
 Ni Binti Mdogo mwenye umri wa miaka 12 na mwenye upeo mkubwa Zurpha Issa yeye alitaka kujua ni namna gani anaweza vipi kujizuia na mabadiriko yake? ambapo pia alieleza kuwa yeye anandoto ya kuwa msanii hapo baadae.
Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi  akifuatilia kwa makini mdahalo huo
Steven Mfuko Maarufu kwa Jina la Babu Zero akichangia mada katika mdahalo huo ambapo alizungumzia changamoto za mabinti kuvunja ungo wakiwa katika umri mdogo na kuelezea namna vijana wanavyo warubuni na kuwadanganya mabinti wadogo.
Muongozaji Mdahalo huo wa Nafasi ya Mtoto wa Kike kwenye Jamii Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa  Ambassador Angelo(wa pili kulia) akiendelea kutoa mwongozo
Bi. Mwafine Kimwaga mkazi wa Tandale akielezea namna alivyo mpokonya simu mwanae kwa kuhofia kuwa inaweza kuwa ni chanzo cha kumharibu kisha kumpa adhabu kali
Bi Stella Francis Mganga akielezea jinsi mabadiliko makubwa ya Teknolojia yalivyo na yanavyo endelea kuporomosha maadili ya vijana wengi na kutumia muda wao mwingi huko kulipo kufanya maswala mengine.
Mhandisi Eliwanjeria James  kutoka Kikundi cha Mainjinia wanawake Tanzania  akichangia mada katika jukwaa hilo
Asha Furaha mkazi wa Tandale akieleza mambo mbalimbali yanayowakabili mabinti na kuwasihi kuendelea kupata elimu zaidi juu ya usichana wao
Madam Sophie Mbeyela akitoa mchango wake wakati wa kujadili mada ya Nafasi ya Mtoto wa kike kwenye jamii
Vijana, Wazazi na wadau mbalimbali wakiwa katika jukwaa hilo
 Picha ya Pamoja
(Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA WATOA ELIMU JUU YA KUDUMISHA AMANI KATIKA FAMILIA, JUKWAA LA VIJANA JIJINI DAR
GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA WATOA ELIMU JUU YA KUDUMISHA AMANI KATIKA FAMILIA, JUKWAA LA VIJANA JIJINI DAR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiJuSLQsa-bbfZ7QjQJa-sZX0px6__H5vsRHJhy_URUngt0f0mmd5d4jFtYHkB9CBH8Kx3eMPrN2_kzqkyuTkkYcLpHs0VnrYp1EoG6pRkzd2ESJT2Dl3ddkpSmofA9CJQLh5CoxM2REO3U/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiJuSLQsa-bbfZ7QjQJa-sZX0px6__H5vsRHJhy_URUngt0f0mmd5d4jFtYHkB9CBH8Kx3eMPrN2_kzqkyuTkkYcLpHs0VnrYp1EoG6pRkzd2ESJT2Dl3ddkpSmofA9CJQLh5CoxM2REO3U/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/10/global-peace-foundation-tanzania-watoa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/global-peace-foundation-tanzania-watoa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy