Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco, Mohammed V...
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco, Mohammed
VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika
na Waislamu wengine wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil
Soraga katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja Oktoba 28, 2016. Mfalme
Mohammed VI yupo visiwani humo kwa ziara ya kibinafsi. (PICHA NA IKULU YA
ZANZIBAR)
Viongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar
Mfalme
wa Morocco, Mohammed VI akisalimiana na Katibu wa Mufti wa
Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia), akipokea mmoja kati ya misahafu 10,000, iliyotolewa na Mfalme wa Morocco,
Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo Oktoba 28, 2016 katika
Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja. Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya
kibinafsi na ujumbe wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani
Mjimkongwe wa Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein
(kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na Mkuu wa Mkoa
wa Mjini Magharibi Mhe, Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakitoka ndani ya Msikiti
wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya Ijumaa.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein
(kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada ya kumalizika
kwa swala ya Ijumaa.
COMMENTS