PANGANI WAPATA KIVUKO KIPYA

  Kivuko Kipya cha Pangani MV. Tanga baada ya kuwasili katika eneo la Pangani Bweni Jijini Tanga.     Kivuko ch...






 Kivuko Kipya cha Pangani MV. Tanga baada ya kuwasili katika eneo la Pangani Bweni Jijini Tanga.
 
 
Kivuko cha Pangani II pamoja na kivuko kipya MV. Tanga vikiwasili katika eneo la Pangani Jijini Tanga. 
 
 
 Abiria na Magari yakiteremka kwenye  kivuko kipya cha pangani MV. Tanga kinachotoa huduma eneo la Pangani Bweni Jijini Tanga. 
 **************
 Na Theresia Mwami-TEMESA
Wananchi wa Pangani na Bweni mkoani Tanga wamepata kivuko kipya cha MV. Tanga, ambacho sasa kitasaidiana na MV. Pangani II kutoa huduma katika eneo la Pangani na Bweni.

Akiongea na wananchi wa Pangani Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Lekujan Manase amesema  kukamilika kwa ujenzi wa kivuko kipya cha MV. Tanga ni muendelezo wa sera ya Serikali ya kuboresha huduma ya vivuko katika maeneo mbalimbali yaliyo na mahitaji ya vivuko nchini. 
 
 
“TEMESA imejipanga kuhakikisha kuwa vivuko vyake vyote vinafanyiwa matengenezo ya kinga kwa wakati, ili kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi wanaotumia vivuko hivyo inapatikana kwa wakati muafaka” Alisema Mhandisi Manase.

Mhandisi Manase ameongeza kuwa  hivi sasa MV. Pangani II itakwenda kwenye ukarabati mdogo na baada ya ukarabati huo vivuko vyote viwili vitabakia katika eneo la Pangani na Bweni ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Lazaro Vazuri  alisema kuwa kivuko cha  MV. Tanga ni mwanzo wa uboreshajji wa huduma ya vivuko nchini na kwa sasa wapo katika mikakati ya kukarabati vivuko vilivyopo na kujenga vivuko vibya ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa vivuko katika maeneo yenye huhitaji.

Mmoja ya wananchi wa Wananchi wa Pangani/Bweni Bw. Othman Juma Ali ameipongeza Serikali kwa juhudi za kupambana na changamoto ya vivuko inayozikumba sehemu nyingi zilizozungukwa na maji.

“Tumekipokea kivuko cha MV. Tanga kwa furaha kubwa na tunaiomba Serikali kutoa huduma ya kivuko hiki kwa saa 24  kila siku ili kitusaidie wananchi hasa wa eneo la Bweni kupata huduma hiyo nyakati za usiku tunapohitaji kupata huduma za kijamii upande wa Pangani” alisema Bw. Othman.

MV. Tanga imesanifiwa na kutengenezwa na Kampuni ya kitanzania ya Songoro Marine Company Ltd na kivuko hiki kina uwezo wa kubeba tani 50 ambazo ni sawa na kubeba abiria 100 na magari 6 kwa pamoja.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PANGANI WAPATA KIVUKO KIPYA
PANGANI WAPATA KIVUKO KIPYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMQZYRSe4694VxCb9wERniSnClIH1qdnaZwtgseQmeFcEeH_EA9x7gosXbCLmEs390d1KdeLn_bAdHt2NqtVg7rVBmtOmYXNjQwei2JFHoX-aexcNLFZ5BKRwmGvwWiHo3mAEIipeSPRq8/s640/PIX+2.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMQZYRSe4694VxCb9wERniSnClIH1qdnaZwtgseQmeFcEeH_EA9x7gosXbCLmEs390d1KdeLn_bAdHt2NqtVg7rVBmtOmYXNjQwei2JFHoX-aexcNLFZ5BKRwmGvwWiHo3mAEIipeSPRq8/s72-c/PIX+2.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/08/pangani-wapata-kivuko-kipya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/08/pangani-wapata-kivuko-kipya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy