ROSTAM AZIZI AFIWA NA BABA YAKE MZAZI, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA JIJINI DAR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano w...
ROSTAM AZIZI AFIWA NA BABA YAKE MZAZI, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA JIJINI DAR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Rostam Azizi, wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay jijini
Dar es Salaam, leo Mei 31, 2014 kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na Baba yake
mzazi aliyefariki katikati ya wiki hii. Kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akijumuika na waombolezaji waliofika nyumbani
kwa Rostam Azizi (kushoto kwa Bilal), Oysterbay jijini Dar es Salaam, Mei 31, 2014 kwa ajili ya
kumpa pole kwa kufiwa na Baba yake mzazi aliyefariki katikati ya wiki hii. Kushoto ni Mufti wa Tanzania, Issa Shaaban Bin Simba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman .
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, akitoa mawaidha wakati wa dua
maalum iliyofanyika nyumbani kwa Rostam Azizi Oysterbay kumuombea Baba mzazi wa
Rostam, aliyefariki katikati ya wiki hii.
Baadhi
ya waombolezaji walioshiriki dua hiyo maalum nyumbani kwa Rostam Azizi. (Picha na OMR)
COMMENTS