Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi sehemu ya vyakula hivyo kwa Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Har...
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi sehemu ya vyakula hivyo kwa Mwenyekiti
wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo aliyepokea kwa niaba ya
vikundi vigine vinne. Mke wa Rais amekabidhi mchele kilo 500, sukari kilo 500
na tende kilo 28, tukio hilo limefanyika katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi sehemu ya vyakula hivyo kwa Mwenyekiti
wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo aliyepokea kwa niaba ya
vikundi vigine vinne. Mke wa Rais amekabidhi mchele kilo 500, sukari kilo 500
na tende kilo 28, tukio hilo limefanyika katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Khalifa
wa Zawiyatul lqadiria, Abas Hamdan watatu kutoka kulia akiongoza dua ya
kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine
wakuu wa serikali mara baada ya tukio la kukabidhi vyakula hivyo. Wengine
katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri mkuu Mama Marry
Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali vya vikundi vya kulea watoto yatima na
watu waishio kwenye mazingira magumu.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na
mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa katika picha ya pamoja na
viongozi mbalimbali wa vikundi vya kulea watoto yatima na watu waishio kwenye
mazingira magumu. Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Mke wa Rais Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mama Mlezi wa Kituo cha Charambe
Islamic Center Asile Zahali mara baada ya kukamilika zoezi la utoaji wa vyakula
mbalimbali kwa vituo vinne vya kulea watoto na watu waishio kwenye mazingira
magumu.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa
akizungumza na viongozi mbalimbali wa vituo hivyo kabla ya kuwakabidhi vyakula
hivyo katika Ofisi yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
*********** ***********
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli amekabidhi chakula kwa ajili ya futari
wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa vituo vinne vya kulea
watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu Jijini Dar es salaam.
Vyakula hivyo vimekabidhiwa leo tarehe 18 Juni, 2016 katika ofisi ya
Mke wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam vimejumuisha Mchele kilogramu 500,
Sukari kilogram 500 na Tende kilogramu 28.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vyakula hivyo, Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli aliyeongozana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
amewatakia heri Waislamu wote katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na
kuwasihi waendelee kuliombea Taifa amani na utulivu.
(“Tunawatakia mfungo mwema wa
mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika kipindi hiki tunawaomba mzidi kuiombea nchi
yetu amani, viongozi wetu wa nchi na watanzania wote kwa ujumla, nchi ikiwa na
amani ndio mambo mengi mazuri yanaweza kufanyika”)
Kwa niaba ya vituo vilivyopatiwa vyakula hivyo, Mwenyekiti wa Kituo cha
Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo amemshukuru Mke wa Rais kwa kutoa
vyakula hivyo na ameeleza kuwa kitendo hicho kinaonesha mshikamano na
ushirikiano walionao watanzania wote bila kujali tofauti ya dini, kabila wala
maeneo wanayotoka.
(“Kwa hiyo ndugu zangu mna imani
ya kikristo lakini mnatambua waislamu ni ndugu zenu, wote tunajenga nyumba
moja, mshikamano ndio tunu tuliyoachiwa na Baba yetu wa Taifa, leo mmeguswa
kuona wenzenu tunafanya ibada na nyinyi mmeingia kwenye ibada, sasa ibada ya kutoa
ni ibada kubwa sana, sio nchi nyingi katika Afrika zinafanya kitendo hiki, watu
hawaelewi, ni nchi chache sana ambazo imani moja inaunga mkono imani nyingine,
lakini sisi waislamu tunalitambua hili hata toka kipindi ambacho mtume wetu SWA
anapigana kusimika dini hii kwa waumini alipata nusura kwa wakristo”)
Vituo vilivyokabidhiwa vyakula hivyo ni Charambe Islamic Center, Tasofe
Lqadiria, Nur Twarigatu Lqadiria na Zawiyatul Lqadiria.
COMMENTS