MAMA JANET MAGUFULI AKIKABIDHIWA CHAKULA NA PANELI ZA SOLA KATIKA KITUO CHA WAZEE BUKUMBI MWANZA

WAZEE na walemavu wa viungo wanaoishi katika mazingira magumu katika kambi ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi mkoani hapa, wamek...





WAZEE na walemavu wa viungo wanaoishi katika mazingira magumu katika kambi ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi mkoani hapa, wamekumbukwa kwa kusaidiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 54.

Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika jana mbele ya mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli katika kambi hiyo yenye watu wenye mahitaji mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alivitaja vifaa vilivyotolewa kuwa ni Mchele tani 6, Unga wa mahindi 6, Maharagwe tani 3, Sukari tani 2 na nusu na mafuta ya kula lita 1000.

Dk. Kimei alitaja vifaa vingine vilivyotolewa katika kambi hiyo ya wazee kuwa ni pamoja na umeme wa jua na kudai kwamba hatawataishia hapo wataendelea kutoa misaada ikiwemo kukarabati majengo ya makazi hayo.

Kwa upande wake, Janet Magufuli, alisema kuwa katika kipindi kichache alichozunguka katika kambi 17 nchini alikuta kambi hizo zinakabiliwa na changamoto nyingine ikiwemo ya maladhi.

Alisema kuwa hali hiyo ilisababisha kuanza kutafuta wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo ambayo ilichukua jukumu hilo la kuwasaidia watu hao, wanaokabiliwa na changamoto nyingi.

Kambi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1974 kwa sasa ina zaidi ya Wazee 100, kwa muda mrefu sasa watu hao wamekuwa ni omba omba katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza.

Vitu hivi endapo kama havita chuchukuliwa hatua na kuwasaidia yanaweza kuwasababishia magonjwa mbalimbali, sasa nilazima wadau wengine wajitokeze kusaidia kambi hizi, alisema mama Magufuli.
Mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli na Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Mwanza, wakati alipowasili katika kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza.
Sehemu ya Misaada iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. 
Mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli (wa pili kulia) akikabidhiwa pannel ya Solar kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, ikiwa ni maalum kwa kusaidia kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magese Mulongo (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mwajuma Nyiruka.
Mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, walipokutana kwenye kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. 
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, akiwasalimia baadhi ya Wazee wanaolelewa kwenye kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. 


Mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli, akiwahutubia wananchi wakati wa hafla ya kukabidhi misaada kwenye kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. 



Mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli (wa pili kulia) akikabidhiwa sehemu ya misaada mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, kwa ajili ya kusaidia kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, akizungumza.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAMA JANET MAGUFULI AKIKABIDHIWA CHAKULA NA PANELI ZA SOLA KATIKA KITUO CHA WAZEE BUKUMBI MWANZA
MAMA JANET MAGUFULI AKIKABIDHIWA CHAKULA NA PANELI ZA SOLA KATIKA KITUO CHA WAZEE BUKUMBI MWANZA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyQxSkvy8w2GJdUFXJQy5dO8B4s34nAFC8JTFZs-Akihekx5CyzBWQJyetel8cua4mrHux_KU-N60yNOcRAMHq6z8R2u8TV4te0KlDI_iaIXHQ3ai-T7ooj_mPMPn0KiKYQPLGDeqSNPPx/s640/_70A1646.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyQxSkvy8w2GJdUFXJQy5dO8B4s34nAFC8JTFZs-Akihekx5CyzBWQJyetel8cua4mrHux_KU-N60yNOcRAMHq6z8R2u8TV4te0KlDI_iaIXHQ3ai-T7ooj_mPMPn0KiKYQPLGDeqSNPPx/s72-c/_70A1646.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/03/mama-janet-magufuli-akikabidhiwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/03/mama-janet-magufuli-akikabidhiwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy