Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwasili Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Kikosi namba 832 Ruvu JKT mkoani ...
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali
wakiwasili Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Kikosi namba 832 Ruvu JKT
mkoani Pwani jana kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za
uzalishaji mali. Kikosi hicho kilichaguliwa kuiwakilisha Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kuonyesha mafanikio ya majeshi
nchini katika shughuli mbalimbali zikiwemo za uzalishaji mali ili kuinua
uchumi wa taifa.
Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu, alikuwa
mgeni rasmi katika ziara hiyo ya siku moja ya waandishi wa habari
kutembelea kikosi hicho. Kingu alimwakilisha Mkuu wa JKT nchini.
Mkuu wa Utawala na
Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion
Kingu (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kutembelea miradi
mbalimbali inayofanywa na kikosi hicho.
Mkuu wa Kikosi 832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge, akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha Mkuu
wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia
Jenelari, Jacob Gedion Kingu kuzungumza na wanahabari katika ziara hiyo.
Mkuu wa Kikosi 832
Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge (kushoto), akiwaelekeza wanahabari
wakati walipofika uwanja wa gwaride kuona vijana wa kidato cha sita
wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wanavyofanya mazoezi ya gwaride la
kuhitimu mafunzo yao ya miezi sita mapema mwezi ujao.
Vijana wa kidato cha sita wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wakionesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
Mary Raphael kutoka mkoani Singida
mmoja wa vijana hao waliopo katika kambi hiyo kwa mujibu wa sheria
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuonyesha jinsi ya
kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
January Sungura (kulia), akizungumza na wanahabari baada ya kuonesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
Gelemaya Kibuga akizungumza na wanahabari.
Dk. Meja Agustino Maile akiwaeleza
wanahabari mambo yanafuatwa kabla ya kumnyoa mteja katika saluni ya
kisasa iliyopo katika kikosi hicho kwa kuzingatia afya na kuepuka
maambukizi ya magonjwa mbalimbali.
Vijana wa mujibu wa sheria wakisubiri kunyolewa katika saluni hiyo.
Unyoaji katika saluni hiyo ukiendelea.
Rehama Hashim muuza wa duka katika kikosi hicho akiwaeleza wanahabari bidhaa zinazopatikana katika duka hilo.
Hapa ni eneo la kiwanda cha kushona nguo ambapo vijana wanaopitia jeshi hilo kwa mujibu wa sheria wanapata mafunzo.
Wanahabari wakiangalia bweni
lililojengwa kwa nguvu ya kikosi hicho kwa ajili ya kukabilana na uhaba
wa vyumba vya kulala vijana hao.
Wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu
wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia
Jenelari, Jacob Gedion (katikati waliokaa mbele), pamoja na maofisa wa
jeshi kutoka Makao Makuu ya JKT na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa na Maofisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo.
Vijana hao wakipiga kwata mbele ya wanahabari na mgeni rasmi.
Vijana hao wakionesha onyesho la kuruka vikwazo.
Onyesho la kuruka vikwazo likiendelea.
Hapa wakiendelea kuruka vikwazo.
Ni Gwaride bila ya kutumia bunduki.
Wanahabari wakiangalia Intaneti
iliyojengwa kwa nguvu ya kikosini hicho kwa ajili ya kusaidia wanafunzi
kuona matokea yao pamoja na mambo mengine ya masomo yao.
Vijana wakiwa katika intaneti hiyo.
Wanahabari wakiangalia mradi wa kuku wa nyama uliopo katika kikosi hicho.
Daktari wa Mifugo, Luteni Ezekiel Mtani (kushoto), akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu mradi wa kuku uliopo kikosini hapo.
Kuku wanaofugwa kikosini hapo wakiwa katika banda maalumu.
Wanahabari wakiangalia mabwawa ya samaki.
Msimamizi wa mradi wa samaki katika
kambi hiyo, Luteni Kelvin Ngodo (katikati), akitoa maelezo ya mradi huo
kwa waandishi wa habari.
Moja ya bwawa la samaki
Bwana shamba wa kikosi hicho, Ndabemeye
Ludovick Rwikima (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu mradi wa
shamba la matunda kikosini hapo.
Bata maji wanaofugwa kikosini hapo wakiwa kwenye banda lao.
Msimamizi wa mradi wa bata maji Rachel Muuta (kushoto), akitoa maelezo kwa wanahabari.
Kilimo cha Vitunguu si Ilula pekee hata Ruvu JKT kinafanyika. Vijana wa JKT wakipalilia vitunguu.
Msimamizi wa shamba la vitunguu, Koplo Robert Eliezer (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilimo cha vitunguu.
Utunzaji Mazingira. Wanahabari wakiangalia shamba la miti iliyipandwa na viongozi mbalimbali katika kikosi hicho.
Wanahabari wakiingia ulipo mradi wa usagishaji nafaka uliopo katika kikosi hicho.
Shughuli za usagishaji nafaka ukiendelea. usagishaji huo unafanywa na vijana wa JKT kwa mujibu wa sheria.
Wanahabari wakinagalia mradi wa usagishaji wa vyakula vya mifugo.
Burudani mbalimbali zikiendelea kutolewa na vijana hao.
Wanenguaji wa bendi ya JKT katika kikosi wakishambulia jukwaa.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Luteni Kanali, Juma Sipe, akizungumza na wanahabari baada
ya kumalizika kwa ziara hiyo ambapo aliwaomba wanahabari kuwa na
ushirikiano na jeshi.
Mwakilishi wa wanahabari hao, Mwanahabari Kibwana Dachi, akitoa neno la shukrani baada ya kumalizika kwa ziara hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
COMMENTS