Baadhi ya wadau wa muziki wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Tabora Jazz, marehem...
Baadhi ya wadau wa muziki wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Tabora Jazz, marehemu Shem Karenga wakati wa maziko yake kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo alasiri.
(Chini na juu) Ni taswira mbalimbali za wanamuziki, marafiki ndugu na jamaa waliojitokeza kumzika gwiji huyo wa muziki aliyezikwa leo jijini Dar es Salaam.
Ankali Michuzi alipokutana na mdau Ali Choki kwenye maziko hayo.
![]() | |||
| (Picha kwa hisani ya Globu ya Jamii ) ***************
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa
Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara
kuomboleza kifo cha mwanamuziki mkongwe, Shem Ibrahim Karenga kilichotokea tarehe
15 Desemba, 2014 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam alikokuwa
amepelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa shinikizo la damu.
Enzi
za uhai wake, Marehemu Karenga alijaaliwa kipaji cha muziki hususan upigaji wa
gitaa la solo na uimbaji, kipaji ambacho kilimwezesha kufanya kazi katika bendi
mbalimbali za muziki hapa nchini akianzia na Bendi ya Lake Tanganyika Jazz mwaka 1964, na baadaye Bendi Maarufu ya Tabora Jazz ikijulikana zaidi kama Wana Segere Matata.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa
sana kutokana na taarifa za kifo cha Mwanamuziki huyu Mkongwe na Mahiri ambaye,
kupitia kipaji alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu, alitoa mchango mkubwa katika
kuiletea sifa nchi yetu”, amesema Rais Kikwete
katika Salamu zake za Rambirambi.
“Kutokana na msiba huu mkubwa, pokea salamu
zangu za rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza mmoja wa Wasanii
Mahiri katika Taifa letu, na kupitia kwako naomba salamu zangu ziwafikie
wasanii kote nchini kwa kumpoteza mwenzao”, ameongeza
kusema Rais Kikwete akiomboleza msiba huo.
Rais
Kikwete ametoa salamu za pole kwa familia ya marehemu Karenga kwa kupoteza
kiongozi na mhimili wa familia. Amewaomba wanafamilia wawe wavumilivu na
watulivu wakati huu wanapopitia kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa
wao, na anamuomba Mola aipokee na aiweke mahala pema peponi roho ya Marehemu
Shem Ibrahim Karenga, Amina.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
16 Desemba,2014
|



































COMMENTS