TANZANIA INA MZIGO MKUBWA WA MAGONJWA WA KISUKARI NA MADHARA YA UNGONJWA WA KISUKARI KWENYE MIGUU. Waziri wa Afya na Ustawi ...
TANZANIA INA MZIGO MKUBWA WA MAGONJWA WA KISUKARI NA MADHARA YA UNGONJWA WA KISUKARI KWENYE MIGUU.
Dr.
Zulfiqarali G. Abbas, Consultant Physician,
Mwenyekiti
Pan African Diabetic Foot Study Group.
Tanzania ina mzigo mkubwa wa magonjwa wa kisukari na madhara ya
ungonjwa wa kisukari kwenye miguu
Tanzania ina mzigo mkubwa wa magonjwa yasiyoambukiza,
sio tu kisukari bali na matatizo yanayoambatana na ugonjwa huu kama vile
vidonda vya kisukari miguuni, ambalo ongezeko lake haliwezi kufumbiwa macho.
Haya yalisemwa na mwenyekiti wa Pan African Diabetic Foot Study Group na pia
mwenyekiti wa mradi wa miguu wa Step by Step. Dr. Zulfiqarali G. Abbas. Daktari
wa Hospitali ya Taifa na Chuo kikuu cha Afya cha Muhimbili. Akizungumza hayo
wakati wa Mkutano wa pili wa Pan African Diabetic Foot study Group uliofanyika
katika hotel ya Blue Pearl jijini Dar es salaam, kuanzia tarehe 24 Agosti mpaka
tarehe 26 Agosti. Ambao ulifunguliwa na Waziri wa Afya mheshimiwa Dr. Seif
Rashid. ( Ripota)
Tulifanya
mahojiano na Dokta Abbas juu ya mafanikio ya mkutano huu wa kimataifa kuhusu
vidonda vya kisukari miguuni, jijini Dar es salaam.
Daktari Abbas alisema wajumbe kutoka kila sehemu duniani
waliwasili. Wapo wajumbe kutoka nchi tisa nje ya bara la Africa, wajumbe
ishirini na tisa kutoka nchi za Africa. Na wajumbe kutoka mikoa ishirini na
sita ya Tanzania. Mkutano huu wa kimataifa wa cku tatu. Malengo ya awali
kutokana na mkutoano huu ni ni kutoa taarifa zilizopo kwa wakati huu kuhusiana
na kinga na matibabu juu ya vidonda vya kisukari miguuni katika Africa.
Wasemaji tofauti ambao wapo kwenye Nyanja hii ya vidonda vya kisukari miguuni
watawasilisha hotuba adilifu. Mbali na hotuba hizo pia kutakuwa na maonyesho ya
vitendo jinsi ya kuhudumia vidonda vya kisukari miguuni.
Tumekusanya
vipindi vya kuvutia vya kisayansi, maelezo yenye ushahidi ndani yake ambayo
yameleta maboresho katika utunzaji wa vidonda vya kisukari miguuni. Matibabu
yanayofanyika katika nchi za Africa. Tunazo hotuba arobaini kutoka kwa wataalam
wa miguu na vipindi nane vya elimu ya vitendo juu ya vidonda vya kisukari
miguuni.
Daktari
Abbas alisema kisukari ni
ugonjwa sugu ambao unahitaji juhudi za haraka kuukabili. Mwaka 2013, makadirio
ya dunia nzima yalifikia idadi ya milioni 382. Idadi hii inatarajiwa kuongezeka
na kufikia milioni 592 sawa na ongezeko la asilimia (55%) ifikapo mwaka 2035.
Katika bara la Afrika mwaka 2013 idadi ilifikia milioni 19.8 ambapo inatarajiwa
kuongezeka mpaka milioni 41.4 mpaka ifikapo mwaka 2035. Na wakati huohuo
madhara ya miguu yataongezeka. Kila sekunde 20 kiungo cha binadamu kinapotea
kutokana na ugonjwa wa kisukari. Inakadiriwa kuwa asilimia 15% ya wagonjwa wote
wa kisukari wataathirika na vidonda vya miguu katika maisha yao. Kiasi cha
asilimia 85% ya ukatwaji wa viungo kwa watu wa kisukari inachangiwa na vidonda
vya miguuni.
Alianza
kwa kusema kuwa elimu ndio kinga kubwa juu ya vidonda kwa watu wenye kisukari.
Kuna umuhimu wa haraka sana ili kuongeza elimu kwa wale wote wanaohusika na
matibabu ya kisukari. Mahitaji ya haraka juu ya elimu ya vidonda vya kisukari
miguuni, mafunzo ya muda mfupi kwa nchi zinazoendelea. Mafunzo kama hayo
yameimarishwa na yanafuatiliwa na kufanyiwa tathmini kwa wakati. Daktari
Zulfiqarali G. Abbas mtaalamu aliyebobea katika ugonjwa wa kisukari, pia
mwenyekiti wa Pan African Diabetic Foot Study Group na mradi wa miguu wa Step
by Step, unaoshughulikia vidonda vya kisukari miguuni. Ameratibu vipindi
tofauti vya mafunzo pamoja na kuona wagonjwa wengi wa vidonda vya miguu.
Daktari Abbas amejiwekea lengo katika maisha: Kuboresha matibabu yanayotolewa wa watu wa kisukari wenye vidonda vya
miguu nchini Tanzania.
Swali: Takwimu zinaeleza
nini juu ya ugonjwa wa kisukari?
Dr. Z. G. Abbas
Mwaka
2011, makadirio ya ugonjwa wa kisukari duniani ilikuwa milioni 366 (sawa na
kiwango zaidi ya asilimia 8.3 ya watu wazima duniani kote.)
Imetabiriwa
kwamba idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari itaongezeka na kufikia
watu milioni 552 ifikapo mwaka 2030.
Kila
dakika nane (8) mtu mmoja anakufa kutokana na ugonjwa wa kisukari duniani.
Kisukari ni moja ya sababu kumi zinazoleta ulemavu, ambapo huleta madhara zaidi
ya upofu pamoja na upotevu wa viungo vya mwili.
Hali
katika bara la Afrika ni kwamba katika mwaka 2010 – watu milioni 12.1 wanaugua
ugonjwa wa kisukari, na idadi hii itazidi mara mbili itakapofikia mwaka 2030.
Hili ni ongezeko la asilimia 98.1%.
Swali: Vipi kuhusu
takwimu juu ya matatizo ya miguu kutokana na ugonjwa wa kisukari duniani?
Dr. Z. G. Abbas
Na
katika kila sekunde thelathini (30) mgonjwa mmoja wa kisukari hukatwa mguu,
hivyo katika kila dakika moja (1) watu wawili hukatwa miguu kutokana na athari
za kisukari. Na hivyo kufanya kila masaa mawili, watu mia mbili arobaini (240)
hukatwa mguu.
Duniani
kote, asilimia 40-60% ya ukatwaji wa viungo haswa miguu bila kupata ajali,
hufanyika kwa watu wenye kisukari. Katika madhara yote yanayohusiana na ugonjwa
wa kisukari, matatizo ya miguu ni yenye hatari na gharama zaidi. Taarifa juu ya
janga hili zimeonyesha kuwa katika kipindi cha miaka sita iliyopita ukatwaji wa
viungo milioni moja umekuwa ukiwakumba watu wenye kisukari kila mwaka.
Makadirio haya yalipendekeza kuwa mguu mmoja unakatwa katika kila sekunde
thelathini sehemu fulani duniani. Wakati makadirio ya vifo yanayohesabika kwa
kutumia viwango vya taarifa zilizotolewa mwaka 2011, imeonekana kwamba kila
sekunde ishirini duniani kiungo kimoja kinakatwa kutokana na ugonjwa wa
kisukari.
Swali: Nini lengo la
mradi huu wa miguu wa step by step – kuboresha utunzaji wa miguu katika nchi
zinazoendelea?
Dr. Z. G. Abbas
Elimu
ni mojawapo ya nguzo muhimu katika kukinga vidonda vya kisukari miguuni. Yapo
mahitaji ya haraka kuongeza ufahamu kwa watoaji huduma katika ugonjwa wa
kisukari. Uhitaji wa elimu endelevu juu ya vidonda vya kisukari miguuni na tiba
programu ya mafunzo mafupi chini kwa nchi zilizoendelea. Mafunzo haya yamewekwa
na yamekuwa na mafanikio makubwa na yamekuwa yakisimamiwa na kutathminiwa na
maendeleo ya vyanzo vya ufundishaji.
Malengo na Makusudio ya
Mradi Huu:
Kujenga
ufahamu zaidi juu ya vidonda vya kisukari miguuni katika nchi zinazoendelea. Kuzalisha
mafunzo imara kwa wataalamu wa afya katika kusimamia vidonda vya kisukari
miguuni. Kusaidia katika upatikanaji wa taarifa kutoka wa wataalam wa afya
waliopitia mafunzo kwa wataalam wengine wa afya na hivyo kupelekea umahiri
zaidi. Kupunguza hatari zinazopelekea matatizo ya viungo kwa wagonjwa wa kisukari.
Kuwawezesha watu wenye kisukari kutunza miguu yao, kugundua matatizo mapema na
kutafuta msaada mapema mara wapatapo matatizo.
Mradi
huu ni kwa nchi zilizoendelea katika kupunguza ukatwaji wa viungo kwa asilimia
50%. Mradi huu unaitwa Step by step project. Mradi huu umedhaminiwa na Chama
Cha Kisukari Duniani (WDF). Viongozi wa kitaalamu ni kutoka Chuo Kikuu Cha
Sayansi ya Afya Muhimbili (MUCHS), Kongamano la Kimataifa la Kisukari (IDF),
Diabetic foot society of India, na International Working Group on the Diabetic
Foot (IWGDF). Kwa sasa tayari tumeshatoa
mafunzo kwa madaktari kutoka vituo 45 na kwa madaktari wa upasuaji kutoka vituo
20 kupitia mradi huu kote nchini.
Mradi
umeratibiwa kwa miaka miwili. Sehemu ya kwanza ilikuwa mafunzo ya msingi katika
utunzaji wa miguu na kisha mafunzo ya juu zaidi. Madaktari na wauguzi ni kutoka
katika hospitali za wilaya na hospitali za binafsi kwa vituo 45 nchini kote,
ambavyo vinajishuhulisha na huduma za ugonjwa wa kisukari.
Mradi
wa step by step mara ya kwanza ulianzishwa nchini Tanzania na India kama mradi
kiongozi mwaka 2004. Tulibahatika kupata mradi huu nchini kwetu. Kutokana na
mafanikio yake, leo mradi kama huu umeanzishwa katika nchi nyengine
zinazoendelea. Mradi huu umefanikiwa katika malengo yake upande wa elimu na
tumepeleka na kuratibu mafunzo katika nchi kama Pakistan, Egypt, Visiwa vine
vya Carribean, Congo, Guinea. Na pia mafunzo haya yanategemewa kufanyika katika
nchi nyengine zinazoendelea. Dhumuni kubwa ni kupunguza kiwango cha ukatwaji wa
viungo kwa asilimia hamsini 50%. Timu za madaktari na wauguzi wanapata elimu
hivyo watakaporudi katika vituo vyao vya afya watoe elimu waliyopata kwa watoa
huduma za afya wenzao, ili nao waweze kutoa kwa wagonjwa wao. Elimu hii
endelevu ni moja ya muonekano muhimu wa mradi huu yaani elimisha waelimishaji.
Awali
ya yote lengo kubwa la mradi huu ni kujenga ufahamu kati ya watu wenye
kisukari, jamaa pamoja na ndugu zao. Pili, kuhakikisha wataalam wa afya wana
ufahamu juu ya tatizo hili la ugonjwa wa kisukari kwenye miguu. Mwisho, kiwango
cha ukatwaji wa viungo kimepungua kote nchini tangu kuanzishwa kwa mradi huu
muhimu wa Step by Step.
Swali: Je, Kuna utafiti
wowote uliofanyika nchini Tanzania juu vidonda vya kisukari na ukatwaji wa miguu.
Dr. Z. G. Abbas
Ndio,
utafiti uliofanyika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili unaonyesha kuwa:
Asilimia
kumi na tano (15%) ya wagonjwa wa kisukari wanaolazwa hospitalini hapo ni
kutokana na matatizo ya miguu. Asilimia themanini (80%) ya wagonjwa hawa wenye
vidonda miguuni ndio wanaonwa kwa mara ya kwanza wakiwa na tatizo la vidonda
miguuni. Asilimia thelathini na tatu (33%) wanaolazwa kutokana na kisukari,
huishia kukatwa viungo ili kuyanusuru maisha yao. Sababu ya kiwango kikubwa cha
ukatwaji wa viungo ni kwamba wagonjwa hawa hufika hospitalini wakiwa katika
hatua mbaya zaidi. Iwapo wagonjwa wa kisukari wataweza kufika hospitalini
haraka kwa ajili ya matibabu, wanaweza kunusurika kupoteza viungo au maisha.
Mara nyingi ukatwaji wa miguu hutokana mchanganyiko wa maambukizi ya hali juu,
uharibifu wa mishipa ya fahamu, pamoja na upungufu wa damu miguuni. Watu wenye
kisukari hulazwa hospitalini muda mrefu kutokana vidonda vya miguu,
kulinganisha na matatizo mengine yanayotokana na ugonjwa wa kisukari. Kiwango kikubwa cha matatizo ya miguu kina
nafasi kubwa katika jamii ya watu wenye kisukari na pia katika hesabu za afya.
Ni muhimu kujua matatizo ya miguu yanatokeaje, na jinsi gani ya kuepukana na
pia kuyagundua mapema ili matibabu yawe yenye kufanikiwa.
Swali: Kisukari kinawezaji
kuathiri miguu yako?
Dr. Z. G. Abbas
Watu
wenye kisukari wanaishi katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya miguu
kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kuharibu mishipa ya damu na mishipa ya
fahamu, hali inayopelekea ukosefu wa hisia miguuni. Kutokana na hali hiyo,
maumivu na mikandamizo hutokea bila kujua, hali hii huruhusu matatizo kutokea
bila ya mtu kujijua.
Uharibifu wa Mishipa ya Fahamu (Neuropathy)
Kisukari kama kilivyo ikiwa hakijatawaliwa vizuri, kinaweza
kuharibu mishipa ya fahamu nyayoni na miguuni. Uharibifu wa mishipa ya fahamu
ni tatizo sugu kwenye kisukari. Uharibifu huu wa mishipa ya fahamu huitwa neuropathy. Uharibifu wa mishipa ya fahamu unapotokea, hupelekea
miguu kukosa raha, kutohisi maumivu au kukosa hisia hali inayosababisha miguu
kuwa na ganzi. Dalili zake ni pamoja na kuhisi nyayo kuwaka moto,
kuchomwachomwa, ganzi, na misuli kukaza miguuni. Bahati mbaya, ikiwa huwezi
kuhisi maumivu unaweza kuwa katika hatari ya kupata majeraha bila ya wewe
kujua. Na hii ndio sababu kubwa ya vidonda vya miguu katika jamii yetu. Kidonda
kitatengeneza njia ya maambukizi, ambayo itapelekea kidonda kutokupona, na
kuoza hali itakayopelekea mguu kukatwa.
Vidonda vya moto kutokana na
uharibifu wa mishipa ya fahamu uliosababishwa na Ugonjwa wa Kisukari. (Diabetic
Neuropathy)
Udhaifu katika mzunguko wa damu.
Mishipa ya damu miguuni ina tabia ya
kuwa myembamba hivyo damu kushindwa kufika miguuni kwa urahisi. Hii huitwa ”ischemia”. Iwapo mzunguko ni dhaifu,
ngozi yenye jeraha inaweza isipone kwa urahisi. Kupungua kwa mtiririko wa damu
hupelekea upungufu wa hewa ya oxygen na virutubisho miguuni, ambayo kuchelewa
kupona au kutokupona kabisa. Kuziba
kabisa kwa mishipa ya damu husababisha ngozi kufa. Hali hii huitwa ”gangreen”. Uvutaji wa sigara husababisha
mtiririko kuwa mbaya zaidi haswa ukiwa na kisukari. Hivyo inasisitizwa kuacha
kuvuta sigara ikiwa ni mvutaji.
Maambukizo.
Kisukari kinaweza kupunguza uwezo wa
mwili kupambana na maambukizi. Hii inamaanisha kuwa sio tu miguu inakuwa katika
hatari ya maambukizi, bali pia inakuwa sio kazi rahisi kuua maambukizi mara tu
yanapoingia. Maambukizi yanaweza kusambaa na pia yasigundulike kwa urahisi
mpaka kufikia hatua mbaya. Hivyo ni muhimu kutibia maambukizi kwa antibiotic
haraka iwezekanvyo.
Mambukizo makubwa
yaliyopelekea kukatwa kwa miguu
Swali: Ni zipi dalili za hatari, ambazo ungewaeleza wagonjwa wako?
Dr. Z. G. Abbas
Ni muhimu kwa wagonjwa wenye
kisukari kumuona daktari mara wagunduapo hali yoyote kati ya hizi zifuatazo.
Iwapo mgonjwa atachelewa kutoa taarifa anaweza kuishia na matokeo mabaya. Zifuatazo
ni dalili muhimu za hatari:
- Uvimbe katika miguu au unyayo.
- Mabadiliko ya umbo au kipimo cha mguu au unyayo
- Miguu au nyayo zinapata baridi sana.
- Mabadiliko ya rangi nyekundu, blu au nyeusi.
- Vidonda hata viwe vidogo kiasi gani.
- Majeraha yasiyopona.
- Kucha zinazoota kwenda ndani ya nyama ya kucha.
- Kuwa na Sugu.
- Ukosefu wa vinyweleo miguuni.
Swali: Ni muongozo gani wa msingi katika utunzaji wa miguu ungependa
kuwaeleza wagonjwa wenye kisukari?
Dr. Z. G. Abbas
Uchunguzi wa miguu kila siku:
Hakikisha unachunguza miguu yako
mara moja kwa kuangalia iwapo kuna mabadiliko ya rangi, vidonda, mipasuko,
michubuko, au jeraha. Tumia kioo kuona sehemu ya unyayo.
Usafi:
Safisha miguu yako kila siku.
Usiroweke miguu kwenye maji. Kausha miguu yako vizuri haswa katikati ya vidole kila umalizapo kuoga.
Utunzaji wa kucha:
Iwapo unakata kucha zako jaribu:
Kuzipunguza kwa uangalifu, fuata
umbile la kucha. Majeraha yatokanayo na ukatwaji wa kucha yanaweza kupelekea
maambukizi na vidonda. Usikate pembezoni mwa kucha. Usikate kucha zikawa fupi
sana. Chonga kucha kurekebisha kingo za kucha.
Usikate kucha zako iwapo:
- Macho hayaoni vizuri
- Miguu ina ganzi
- Mtiririko wa damu sio mzuri
- Kucha zako ni nene na .ngumu sana.
Ngozi:
- Kisukari hupelekea ngozi kuwa kavu, hivyo kupasuka kwa urahisi.
- Hivyo tumia cream ya kulainisha ngozi kila siku.
- Usitumie cream ya kulainisha ngozi katikati ya vidole.
- Chunguza ngozi kwa ajili ya michano, malengelenge, au mipasuko kila siku.
- Sugu zikatwe na daktari.
- Usitumie plasta au kemikali kuondoa sugu.
- Usitumie chochote kwenye ngozi bila ushauri wa daktari.
Viatu :
Ni muhimu viatu vyako viwe sahihi
kwa miguu yako, sababu viatu imekuwa ni moja ya sababu kubwa ya majeraha.
Chunguza ndani ya viatu vyako iwapo kuna kitu chochote cha hatari kama misumari
au mawe na mikwaruzo kwenye viatu kabla ya kuvivaa. Hii inaweza kuleta muasho,
jeraha, au hata vidonda miguuni. Kinga miguu yako kwa kuvaa viatu wakati wote.
Vitu vya moto au baridi:
Epuka padi za kupashia joto, chupa
za maji moto au tyubu za maji moto miguuni mwako. Upungufu wa hisia huweza
kupelekea kuungua, au kupata malengelenge bila ya kuhisi maumivu.
Kumuona daktari:
Kama una hisia tofauti kwenye miguu
yako hakikisha unamuona daktari. Hakikisha unazungumza na daktari kuhusu
utunzaji wa miguu pamoja na kuweka sukari katika kiwango kizuri.
****************
COMMENTS