MAZISHI YA MWANAHABARI NGULI NCHINI MZEE NKWABI NG'WANAKILALA Mhariri wa gazeti la ThisDay, Fumbuka Ng’wanakilala (aliyebeba msa...
MAZISHI YA MWANAHABARI NGULI NCHINI MZEE NKWABI NG'WANAKILALA
 |
| Mhariri wa gazeti la
ThisDay, Fumbuka Ng’wanakilala (aliyebeba msalaba), pamoja na wadogo zake,
Lugendo (kushoto) na Manyanda (kulia), wakiwaongoza
waombolezaji waliobeba jeneza lenye mwili wa Baba yao, marehemu Mwl. Nkwabi
Ng’wanakilala baada ya kuwasili nyumbani kwao Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar
es Salaam Julai 01 mwaka huu, kwa ajili mazishi. Mwl. Ng’wanakilala, ambaye alikuwa Mhadhiri
katika Idara ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Augustino (SAUT), jijini Mwanza alifariki Juni 27, katika Hospitali ya Bugando
baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo na tumbo. |
 |
| Nkwabi Ng'wanakilala enzi za uhai wake. |
 |
| Ndugu, jamaa na
waombolezaji wakilitelemsha jeneza lenye mwili wa Mwl. Ng’wanakilala kutoka
kwenye gari baada ya kuwasili nyumbani Kibamba. |
 |
| Sehemu ya
waombolezaji wakiwa msibani Kibamba. |
 |
Baadhi ya wadau wa Habari wakiwa kwenye mazishi ya mwana habri nguli huyo. (PICHA ZOTE/JOHN BADI)
|
COMMENTS