IPTL YAPIGA JEKI UJENZI WA KITUO CHA POLISI CHA MBWENI- MALINDI Meneja Mkuu wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la Polisi ...
IPTL
YAPIGA JEKI UJENZI WA KITUO CHA POLISI CHA MBWENI- MALINDI
Meneja
Mkuu wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la Polisi la Tanzania, Kamishna
wa Polisi Thobias Andengenye (kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Bw.
Harbinder Sethi (kushoto), wakati akipokea hundi ya shilingi milioni 10
iliyotolewa na IPTL kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi cha
Mbweni-Malindi. Katikati ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum la kipolisi
Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova.
Meneja
Mkuu wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la Polisi la Tanzania, Kamishna
wa Polisi Thobias Andengenye (kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni
10 Kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Independent Power
Tanzania Limited (IPTL), Bw. Harbinder Sethi (kushoto) iliyotolewa na
kampuni yake kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi cha Mbweni-Malindi. Katikati ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum la Kipolisi Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova.
====== ========
KAMPUNI
ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imepiga
jeki mradi wa ujenzi wa kituo cha polisi cha Mbweni Malindi kwa
kuchangia zaidi ya silingi milioni 10, ikiwa na lengo la kuyafanya
maeneo hayo kuwa maeneo salama kibiashara.
Wakati
akikabidhi mchango huo kwa maafisa wa polisi kanda maalum la kipolisi
Dar es Salaam katika eneo la ujenzi mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti
Mtendaji wa IPTL, Harbinder Sethi alisema kampuni yake imeitikia wito wa
kusaidia ujenzi huo sababu inaamini kuwa usalama thabiti utasaidia
maendeleo ya haraka kiuchumi katika eneo husika.
“IPTL
inaelewa kuwa ili kupata maendeleo thabiti ya kiuchumi katika sehemu
yoyote ile, ni lazima eneo hilo liwe na usalama wa kutosha. Utakapo
boresha usalama, wawekezaji wataleta fedha sababu watakuwa na uhakika
kuwa fedha zitakuwa salama. “Ongezeko la uwekezaji katika jamii pia litabadilisha hali ya kiuchumi na maisha ya watu.
Hii
ndiyo maana tumetenga sehemu ya pato letu ili kusaidia miradi mbali
mbali ya kijamii ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia miradi ya
kijamii inayotuzunguka,” alisema.
Bw.
Sethi alisema kuwa IPTL imejikita katika kusaidia miradi mbali mbali
yenye chachu kubwa ya kuwaletea watu maendeleo ya kiuchumi na kijamii
kwa ujumla.
Akipokea
hundi hiyo kwa niaba ya Jeshi la Polisi, Meneja Mkuu wa Utawala na
Rasilimali katika Jeshi la Polisi la Tanzania, Kamishna wa Polisi,
Thobias Andengenye alisema mchango huo utasaidia kukamilisha mradi huo
utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 700. “Kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu, napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa mchango huu.
Ninaamini
kwamba baada ya mradi huu kukamilika na kuzinduliwa, uwepo wa polisi
utasaidia kuboresha hali ya usalama katika eneo hili la Mbweni. Kama
mnavyofahamu, hakuna maendeleo ya kiuchumi yanayoweza patikana katika
eneo lisilokuwa na usalama. Tunakushukuruni sana,” alisema.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo hicho cha polisi,
Reeves Mutalemwa alisema maombi ya ujenzi wa kituo hicho cha polisi
yalitumwa na wakazi wa Mbweni ambao pia wamekuwa wakichangia katika
mradi. (Imeandaliwa na Michuzi JR)



COMMENTS