KINANA ATIA FORA ZIARA YAKE SUMBAWANGA VIJIJINI, MAELFU WAFURIKA MKUTANO KATA YA ILEMBO, AZINDUA NA KUCHAGIA MIRADI YA SHULE, ZAHANATI, KITUO CHA POLISI, MSAFARA WAKE WAZUIWA NJIANI NA WANANCHI

KINANA ATIA FORA ZIARA YAKE SUMBAWANGA VIJIJINI, MAELFU WAFURIKA MKUTANO KATA YA ILEMBO, AZINDUA NA KUCHAGIA MIRADI YA SHULE, ZAHANATI, K...

KINANA ATIA FORA ZIARA YAKE SUMBAWANGA VIJIJINI, MAELFU WAFURIKA MKUTANO KATA YA ILEMBO, AZINDUA NA KUCHAGIA MIRADI YA SHULE, ZAHANATI, KITUO CHA POLISI, MSAFARA WAKE WAZUIWA NJIANI NA WANANCHI MARA KADHAA


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi, katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika  ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa, Aprili 3, 2014.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya watu, katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika  ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa, Aprili 3, 2014. 
 
 Maelfu ya wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Ilembo wilaya ya Sumbawanga vijijini.
 Katika hali inayoonyesha wananchi wengi kuridhishwa na utendaji kazi wa Kinana, mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kiongozi huyo katika kata ya Ilembo wilaya ya Sumbawanga vijijini wakiwa na bango la kusifu uchapakazi huo wa Kinana
 Kinana akimpa kadi ya CCM, mwanachama mpya Eva Thomas, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Ilemba, Sumbawanga Vijijini. Zaidi ya wanachama wapya 250 wa CCM, walikabidhiwa kadi
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Mjumbe wa NEC Balozi Ali Karume wakiingia kwenye Uwanja wa mkutano huo.
 Vijana wa UVCCM wakiimba kwaya wakati wa mkutano wa Kinana, kijiji cha Ilemba
Kinana akifurahia vijana wakati wakicheza ngoma kumlaki alipowasili uwanja wa mkutano katika kata ya Ilembo 
Kinana akisaidia kuweka dirisha kwenye bweni la wasichana Shule ya Sekondari, Ilembo Sumbawanga vijijini wakati wa ziara yake katika wilaya hiyo. 
 Kinana akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga vijijini kwa kufanikisha usimamizi wa ilani ya CCM kwa kujenga bweni hilo la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Kata ya Ilembo wilayani humo. 
Kinana akishiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Ilemba, Sumbawanga vijijini. Ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji na bati 50 kumalizia ujenzi wa kituo hicho.
 Kinana akifungua shina la wakereketwa la vijana wa UVCCM la Makoko, katika Kijiji cha Ilemba.
 Kinana akizindua shina la Vijana la Makoto, Ilemba Sumbawanga vijijini
 Msafara wa Kinana ukipita kwenye mto kutokana daraja kuharibika katika barabara ya kutoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini.
Wananchi wa kijiji cha Milepa A wakimshangilia Kinana baada ya kusimamisha msafara wake wakati akitoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini
 Wananchi wa kijiji cha Mtoisa, wakiwa wamesimamisha njiani msafara wa Kinana wakati akitoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini.
 Vijana wa kijiji cha Kalakala, Kata ya Muze wakisakata ngoma kumpokea Kinana alipowasili eneo hilo akiwa njiani kutoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini.
 Wananchi wa kijiji cha Kalakala, Kata ya Muze wilaya ya Sumbawanga vijijini, wakimshangilia  baada ya kutangaza kuchangia mifuko 100 ya saruji na bati 100 ujenzi wa zahanati ya Kata hiyo.
Kinana akiwashukuru wananchi wa Kata ya Muze baada ya kumlazimisha kuzungumza nao licha ya kufika eneo lao saa moja jioni, wakati akitoka Kata ya Ilembo wilaya ya Sumbawanga vijijini kwenda Sumbawanga mjini.

 Mkazi wa Kijiji cha Muze akinyonyesha mtoto wake wakati akiwa miongoni mwa wananchi wa kijiji hicho waliomlaki Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye kijiji hicho akiwa njiani kutoka Kata ya Ilembo, Sumbawanga Vijijini kwenda Sumbawanga mjini leo, Aprili 3, 2014. (Picha na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KINANA ATIA FORA ZIARA YAKE SUMBAWANGA VIJIJINI, MAELFU WAFURIKA MKUTANO KATA YA ILEMBO, AZINDUA NA KUCHAGIA MIRADI YA SHULE, ZAHANATI, KITUO CHA POLISI, MSAFARA WAKE WAZUIWA NJIANI NA WANANCHI
KINANA ATIA FORA ZIARA YAKE SUMBAWANGA VIJIJINI, MAELFU WAFURIKA MKUTANO KATA YA ILEMBO, AZINDUA NA KUCHAGIA MIRADI YA SHULE, ZAHANATI, KITUO CHA POLISI, MSAFARA WAKE WAZUIWA NJIANI NA WANANCHI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyFZvuBKXuKYBgEiT641dp6IdyqB3cAmWdV2zqo9yjAGluIAqnPaPr7S0SyWA_THB0YONXfL0VjIVcpKk9sp8QvbFNbuQRkfQ-ZV0j516I-HT9x4I1hk7rhYd8FwoyF6O3QLjWHeBpkx2L/s1600/1.+Katibu+Mkuu+wa+CCM%252C+Abdulrahman+Kinana+akihutubia+maelfu+ya+watu%252C+katika+kijiji+cha+Ilemba%252C+kata+ya+Ilemba%252C+wilaya+Sumbawanga+Vijijini+leo+2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyFZvuBKXuKYBgEiT641dp6IdyqB3cAmWdV2zqo9yjAGluIAqnPaPr7S0SyWA_THB0YONXfL0VjIVcpKk9sp8QvbFNbuQRkfQ-ZV0j516I-HT9x4I1hk7rhYd8FwoyF6O3QLjWHeBpkx2L/s72-c/1.+Katibu+Mkuu+wa+CCM%252C+Abdulrahman+Kinana+akihutubia+maelfu+ya+watu%252C+katika+kijiji+cha+Ilemba%252C+kata+ya+Ilemba%252C+wilaya+Sumbawanga+Vijijini+leo+2.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2014/04/kinana-atia-fora-ziara-yake-sumbawanga.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2014/04/kinana-atia-fora-ziara-yake-sumbawanga.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy