KAMPUNI YA JUBILEE WAMKABIDHI SPIKA MAKINDA KADI YA BIMA YA AFYA Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Jubilee, George Alande a...
KAMPUNI YA JUBILEE WAMKABIDHI SPIKA MAKINDA KADI YA BIMA YA AFYA
Afisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Jubilee, George Alande akimkabidhi Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda (kulia) jana, kadi maalum ya bima ya Afya atakayoitumia
kwa ajili ya matibabu baada ya Ofisi ya Bunge kujiunga na kampuni ya
Jubilee Insuarnce kwa ajili ya Bima ya matibabu ya Wabunge wote.
Anaeshuhudia katikati ni Peter Nyabuti kutoka kampuni ya ushauri wa
Bima ya Astra Insurance Brokers.
Spika
Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Bima ya Jubilee, George Alande (kushoto), Peter Nyabuti kutoka
kampuni ya ushauri wa Bima ya Astra Insurance Brokers (kulia) na Kitolina Kippa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya
Bunge.
Afisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Jubilee, George Alande akimkabidhi Mhe. William Lukuvu kadi maalum ya Bima ya Afya atakayoitumia kwa ajili ya
matibabu baada ya Ofisi ya Bunge kujiunga na kampuni ya Jubilee
Insuarnce kwa ajili ya Bima ya matibabu ya Wabunge wote. Anaeshuhudia ni Peter Nyabuti kutoka kampuni ya ushauri wa Bima ya
Astra Insurance Brokers.
Mhe
Lukuvi akiteta jambo na wageni wake ofisini kwake baada ya kukabidhiwa
kadi yake. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu wa Ofisi ya Bunge, Kitolina Kippa (Picha na Owen Mwandumbya)
COMMENTS