MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA ZIARANI SINGIDA KUTEMBELEA VITUO VYA WAZEE WASIOJIWEZA

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msaada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Me...


 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msaada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa tawi la Benki ya NMB Singida, Abius Mlengwa katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017. Kulia ni Mkuu wa mkoa huo, Dkt. Rehema nchimbi.
 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa Tawi la CRDB Manyoni Bw. Richard Karatta katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017. Kulia ni Mkuu wa mkoa huo, Dkt. Rehema nchimbi. (PICHA NA IKULU)

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipowasili wilayani Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa furaha walipowasili katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Afisa Ustawi wa Jamii Yeremia Ngoo akiwapa maelezo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa nyumbani kwa Bibi Agnes Kamota (75) walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na Bibi Agnes Kamota (75) walipomtembelea nyumbani kwake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitembelea  Zahanati ya Sukamahela katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi wakati yeye na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli walipofanya ziara  katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki kucheza ngoma na vikundi vilivyojitokeza kuwalaki katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akihutubia wananchi wakati walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na  mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakioneshana kielele cha kilima cha Sukamahela ambapo inasemekana ndipo ilipo alama ya kuonesha katikati ya nchi ya Tanzania wakati wa ziara yao katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa msaada wa vyakula tani 7.5  katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017

NA MWANDISHI MAALUM
MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.
Wake hao wa viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.
Wameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 13, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Sukamahela wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Katika kituo hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage, ambapo Mama Janeth amewataka viongozi wa kituo kuhakikisha chakula hicho hakichakachuliwi.
Akizungumza na wazee wa makaazi hayo, viongozi mbalimbali na wananchi wanaozunguka eneo hilo Mama Janeth amesema “Naomba chakula hiki kitunzwe vizuri na hakikisheni kinawafikia walengwa na kisichakachuliwe hii ni sadaka,”.
Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulelea walemavu na wasiojiweza nchini kwa sababu wanakabiliwa na changamoto nyingi.
“Watanzania wote popote mlipo tukumbuke kutembelea vituo vya kulelea wazee kikiwepo na hiki tulichokitembelea leo cha Sukamahela na kutoa misaada mbalimbali kkwa kadri tutakavyojaaliwa,” amesema.
Awali Mkuu wa Makazi hayo Bw. Yeremia Ngoo alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuwasaidia watu wenye ukoma na wazee wasiojiweza mkoani Singida.
Bw. Ngoo alisema kituo hicho chenye wakazi 62 kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa wapishi ambapo kwa sasa yupo mmoja huku mahitaji yakiwa ni wapishi wanne. Pia nyumba nyingi ni chakavu na zina nyufa.
Naye Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee Andrea Yohana aliwashikuru wake hao wa viongozi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA ZIARANI SINGIDA KUTEMBELEA VITUO VYA WAZEE WASIOJIWEZA
MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA ZIARANI SINGIDA KUTEMBELEA VITUO VYA WAZEE WASIOJIWEZA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhKPfGGAakwnpX-79LJxOoxxga0GE878shPjm2GY-gSiIvCQYYGt6JJacfLwKGb6bJnSLTZlzs4G6gQB7V_u6gk8ToMZMFthdKmJU-r5RsbyXEMLuWqZaGTvFiL0w3rf7t68dizivbV7Zx/s640/m21.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhKPfGGAakwnpX-79LJxOoxxga0GE878shPjm2GY-gSiIvCQYYGt6JJacfLwKGb6bJnSLTZlzs4G6gQB7V_u6gk8ToMZMFthdKmJU-r5RsbyXEMLuWqZaGTvFiL0w3rf7t68dizivbV7Zx/s72-c/m21.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/mama-magufuli-na-mama-majaliwa-ziarani.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/mama-magufuli-na-mama-majaliwa-ziarani.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy