Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi, Ali Mtopa mara tu baada ya kuwasili kwenye K...
 |
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi Mkoa wa Lindi, Ali Mtopa mara tu baada ya kuwasili kwenye Kata
ya Likunja iliyoko katika wilaya ya Ruangwa ambako zilifanyika sherehe za miaka
37 ya CCM Kimkoa ambapo Mama Salma alikuwa mgeni rasmi tarehe 2.2.2014.
|
 |
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekezwa na Katibu wa Chama Cha
Mapinduzi wa Mkoa wa Lindi, Adeline Gefi sehemu ya kupita ili kupokea
maandamano ya wana CCM na wananchi wa mkoa huo. Wa kwanza kulia ni Dk Maua Daftari, Mlezi wa Chama
Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Lindi.
|
 |
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi, Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi waliofika kwenye sherehe za
kilele hizo.
|
 |
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama
Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akipokea maandamano ya wana CCM na wananchi wa
Mkoa wa Lindi wakati wa sherehe hizo.
|
 |
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua
shina la wakereketwa la Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) katika Kata ya
Likunja wakati wa kilele ya sherehe ya miaka 37 ya CCM zilizofanyika katika
kata hiyo tarehe 2.2.2014. Mara baada ya kuzindua tawi hilo Mama Salma akapokea
shada la maua kutoka kwa mmoja wa viongozi wa UWT wa Kata hiyo na picha ya
mwisho ikiwaonyesha akina mama wajumbe wa Tawi hilo wakishangilia baada ya
uzinduzi huo.
|
 |
Ngoma za utamaduni za makabila
mbalimbali ya mkoa wa Lindi zilishamiri katika hizo. Hata muziki wa kizazi kipya nao uliporomoshwa katika
kilele hicho.
|
 |
Mgeni Rasmi katika sherehe za CCM kutimiza miaka 37
katika Mkoa wa Lindi, Mama Salma Kikwete akikata keki maalum ya sherehe na kuwalisha
wana CCM waliozaliwa mwaka 1977, ambapo CCM kilizaliwa.
|
 |
| Baadhi ya wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Lindi wakisikiliza hotuba
ya mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete wakati wa kilele cha sherehe za kutimiza
miaka 37 ya chama hicho zilizofanyika katika kata ya Likunja, wilayani Ruangwa |
 |
| Mgeni rasmi katika kilele cha sherehe ya kutimiza
miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi, Mkoani Lindi, Mama Salma Kikwete akiwahutubia
mamia ya wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Lindi katika sherehe zilizofanyika
katika Kata ya Likunja, wilayani Ruangwa. |
 |
Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete akiwasisitiza jambo washiriki wa sherehe hiyo. Kulia ni Mbunge Ruhangwa pia Naibu Waziri wa TAMISEMI, Ndugu Kasimu Majaliwa. (Picha na John Lukuwi)
|
COMMENTS