Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, akizima mishumaa. Kulia ni Mkewe Mama Anna na wajukuu wao. Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin M...
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, akizima mishumaa. Kulia ni Mkewe Mama Anna na wajukuu wao. |
Baadhi ya maaskofu wa Kanisa hilo kutoka majimbo mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo. |
Rais mstaafu Benjamin Mkapa akibadilishana
mawazo na Mwenyekiti wa chama Cha NCCRA-Mageuzi, Pia Mbunge wa Kuteuliwa kabla
ya kuanza kwa ibada hiyo.
|
Maaskofu wakiwa katika maadamano pia kuelekea kanisani. |
MTAZIMO WA NDANI WAKATI WA IBADA. |
Kumbukumbu ya pamoja na wanakwaya. |
Kumbukumbu ya pamoja na wanakwaya wengine. |
Mkuu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dk Alex Malasusa akiribishwa na mmoja wa wasimamizi wa kanisa baada ya kuwasili kushiriki ibada hiyo.
|
Picha ya pamoja na mapadri. Wa tatu (kushoto) ni Waziri Mkuu wa mstaafu, David Cleopa Msuya. |
Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin
Mkapa na mke wake Mama Anna wakielekea kwenye maadamano kuingia kanisani.
|
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dk Alex Malasusa wakati wa utambulisho. |
|
Pamoja na wasimamizi wa kanisa. |
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa jana aliadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa kwake kwa kufanya Ibada ya Misa iliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa Katoliki Nchini, Muhadhama Polycarp Kadinali Pengo.
Katika ibada hiyo ya shukrani iliyofanyika Kanisa Katoliki la Immakulata, Upanga jijini Dar es Salaam, Mkapa aliwataka Watanzania kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
“Tunamshukuru Mungu kwa majaliwa
aliyoipatia nchi yetu ya Tanzania na tunamwomba azidi kuijalia umoja
katika yote tunayofanya na tunayokusudia kuyafanya,” alisema Mkapa.
Mkapa pia aliwashukuru waumini
wenzake katika kanisa hilo, huku akifichua siri kwamba, Kadinali Pengo
alimtaka ahamie Kanisa la Mtakatifu Joseph wakati alipokuwa rais, lakini
hakukubali.
Kwa upande wake, Kardinali Pengo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
“Alichofanya Rais Mstaafu Mkapa
ni cha kuigwa. Tunatakiwa kutambua kuwa hatuishi kwa nguvu zetu bali kwa
uwezo wa Mungu hivyo ni lazima tumshukuru kama alivyofanya mwenzetu,”
alisema Kardinali Pengo.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria
ibada hiyo ni pamoja na Mawaziri Wakuu Wastaafu, Edward Lowassa na
Cleopa Msuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa
Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Wengine
ni Mawaziri wa zamani, Sir George Kahama, Bazili Mramba, Profesa Philemon Sarungi, Askofu Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa, Mkuu wa Kanisa la Anglikana Nchini, Dk Valentino Mokiwa, Askofu wa Mtwara, Oscar Mnung'a pamoja wakuu wa
zamani wa Majeshi, Majenerali, Robert
Mboma na George Waitara.
SHEREHE YA MIAKA 75 YA RAIS MSTAAFU, BENJAMIN MKAPA, 'HAPPY BIRTHDAY BEN'
Mandhari
ya ukumbi uliofanyika sherehe ya kumpongeza Rais Mstaafu wa awamu ya
tatu, Benjamin Mkapa ya kutimiza miaka 75, iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Msimbazi Center Dar es Salaam, jana usiku.
Rais
Mstaafu, Benjamin Mkapa, akijumuika na mkewe Mama Anna Mkapa na wana familia yake kukata keki, ikiwa ni ishara ya kupongezwa kwa kutimiza
miaka 75.
Shamra shamra ukumbini wakati wa sherehe hiyo.
Baadhi
ya wageni waalikwa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal, (kushoto) Mama
Zakhia Bilal na baadhi ya viongozi, wakijumuika kumpongeza Mkapa.
Zawadi ya Benjamin kutoka kwa marafiki zake wakaribu.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mawaziri wastaafu na viongozi wa serikali.
Wageni waalikwa.
wageni waalikwa.
Msanii akitoa burudani.
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, akilishwa keki na mkewe Mama Anna Mkapa.
Wakati wa sala katika hafla hiyo.
Baadhi ya wageni maarufu wakiwa katika sherehe hiyo. Kulia ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Mkewe Regina, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim na Mkwewe na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
Mkapa na keki yake.
Ben Mkapa akipongezwa na mke wa Rais, Mama Salma.
WAGENI MAARUFU KATIKA SHEREHE HIYO.
Makamu wa Rais pamoja na wake zake (kulia na kushoto kwake) wakijiandaa kugonganisha glass na Waziri Mkuu mstaafu David Cleopa Msuya (kulia), Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na mkewe Mama Siti wakati wa sherehe hiyo.
Zawadi.......akikabidhiwa mkapa.
Rais Mstaafu Mkapa, akizungumza wakati wa sherehe hiyo.
Makamu wa Rais Dk Bilal, akizungumza kwa niaba ya Serikali.
Makamu wa Rais Dk Bilal. akimpongeza Mkapa.
Picha ya pamoja
COMMENTS