UPDATE KUHUSU HALI MWANDISHI WA HABARI WA ITV UFOO SARO SIMULIZI ZA TUKIO LILIVYOKUWA

UP DATE YA TUKIO LA UFOO SARO, BADO YU CHUMBA CHA DHARURA   Ufoo Saro, baada ya kufanyiwa upasuaji.    Muuguzi wa Hospitali ya T...

UP DATE YA TUKIO LA UFOO SARO, BADO YU CHUMBA CHA DHARURA

 Ufoo Saro, baada ya kufanyiwa upasuaji.
  Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimtoa katika chumba cha Dharula ICU Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV na Redio One, Ufo Saro,  kumpeleka wodini baada ya kumaliza kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi mwilini kutokana na tukio la kujeruhiwa kwa risasi na anayedaiwa kuwa mchumba wake jana alfajiri huko maeneo ya Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
Baadhi ya wanahabari wa vyombo tofauti wakimsindikiza Ufoo na kunasa matukio ya picha zake wakati akipelekwa wodini tayari kwa kulazwa baada ya kufanyiwa upasuaji.
Baadhi ya wanahabari wa vyombo wakimsindikiza Ufoo na kunasa matukio ya picha zake wakati akipelekwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji.

 Mwandishi wa habari wa ITV, aliyejeruhiwa kwa risasi jana asubuhi, alilazimika kuvumilia majeraha ili kujiokoa yeye mwenyewe na wadogo zake watatu waliokuwa wakipigwa risasi, baada ya mama yake mzazi, Anastazia Saro (58), kuuawa.

Mauaji hayo ya kusikitisha, yalifanyika katika eneo la Mbezi Kibwerere, nyumbani kwa mama yake Ufoo ambako alikuwa akiishi na wadogo zake Ufoo ambao ni Goodluck, Innocent na Jonas. 

Matuhumiwa wa unyama huo ametajwa kuwa ni Anthery Mushi, ambaye ni baba mtoto wa Ufoo, na siku ya tukio wawili hao walitokea Mbezi Magari Saba nyumbani kwa Ufoo, kwenda kuzungumza kifamilia na mama mzazi wa mwandishi huyo.
Mushi (40) ni Mhandisi wa kitengo cha Mawasiliano katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini Sudan na aliwasili nchini juzi na kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Ufoo Mbezi Magari Saba.
 

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, Ufoo amejeruhiwa katika paja na tumboni, mama yake mzazi alikufa papo hapo baada ya kupigwa risasi ya kifuani na mtuhumiwa Mushi ambaye naye alijiua baada ya kujipiga risasi kichwani katika eneo la kidevuni.

 Walivyowasili nyumbani 
Akizungumza na wavuti hii jana mdogo wake Ufoo, Goodluck alisema; "Walikuja wakiwa pamoja (Ufoo na Mushi) mapema alfajiri wakiwa ndani ya gari saa 12 kabla ya kuingia ndani walitusalimia kisha wakaingia sebuleni na kuanza mazungumzo na mama."

Goodluck alidai baada ya muda, walisikia milio ya risasi iliyokuwa ikiambatana na sauti ya mama yao akisema "jamani nakufaa," na walipotaka kufungua mlango ili kujua kulikoni, mlio wa risasi uliendelea kusikika kutoka sebuleni. "Pengine muda huo Ufoo ndiyo alikuwa akifyatuliwa risasi," alisimulia.

"Tulipotoka kujua kulikoni, tulimuona dada (Ufoo) akijiburiza chini kuja katika mlango wa chumba tulichokuwa tumelala... akatuambia jifungieni atatuua wote huyu."
"Tulifunga mlango lakini zilipigwa risasi mbili mlangoni huku Mushi akisema tokeni nje niwamalize. Tulitafuta namna ya kujiokoa na kuamua kupanda juu ya dari la nyumba," alisimulia Goodluck.
Kwa mujibu wa madai ya Goodluck, walipanda darini ili kujiokoa kwa kuwa Mushi alifungua ntungi wa gesi na kusababisha hewa kuwa nzito na nahisi alilenga kulipua nyumba ili kuteketeza wote.

"Tulipoanza kupanda juu, alianza kufyatua risasi kupitia dirishani lakini wakati huu alikuwa nje ya nyumba, tunamshukuru Mungu kwani muda huo wote tayari tulikuwa juu kwenye dari tukijaribu kutoka nje ya nyumba na tulipofanikiwa kutoka,tulikmbilia kwa majirani kutoa taarifa," alisema Goodluck.
Hata hivyo alisema majirani walikuja lakini hakuna hata mmoja aliyejaribu kusogelea nyumba hiyo.

Ufoo yuko wapi? 
 Goodluck alisema wakiongozana na askari polisi, waliimgia ndani na kumkuta muuaji akiwa amekaa katika moja ya sofa akiwa tayari amekwisha kufa huku mwili wa mama yao ukiwa sakafuni.
Alisema walijaribu kuangalia ndani kumtafuta dada yao bila mafanikio, ndipo walipotoka nje na na kukutana na mmoja waendesha pikipiki aliyewaeleza kuwa walimuona dada mmoja akiwa ametapakaa damu akiomba kupelekwa Hospitali ya Tumbi.
Alijiandaa 
"Polisi waliingia ndani na kuchukua bastola iliyotumika kwa mauaji pamoja na kuokota maganda ya risasi na wapopekua mfuko aliokuja nao Mushi, ndani yake  walikuta kuna pingu, shoka lenye mpini mfupi pamoja na kamba. Hata hivyo hatukujua alivibeba vitu hivyo kwa sababu gani,"alisema Goodluck.
Alisema baadaye Polisi waliichukua miili ya marehemu wote wawili na kuondoka nayo kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 

Muhimbili
 Ufoo alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana akitokea Tumbi Kibaha, na alifanyiwa upasuaji na juhudi nyingine zilikuwa zikiendelea kuokoa maisha yake.
Hapo jana Mwenyekiti Mtendaji wa IPP , Reginald Mengi aliruhusiwa kumuona Ufoo ambapo alisema anazungumza na hali yake ilikuwa ikiimarika.
Taarifa zilizopatika leo hii kutoka Muhimbili zinaeleza kuwa Ufoo anaendelea vizuri baada ya jitihada za kuondoa risasi mwilini mwake kufanikiwa na hali yake leo inaendelea vyema.
Aidha askari polisi wamegawanyika katika timu tatu, moja Muhimbili, ya pili Kibamba na tatu mtaani kutafuta taarifa muhimu za mauaji. (Imeandikwa na Margreth Itala)


(Imeandikwa na Margreth Itala)





 Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV na Redio One, Ufoo Saro, katika Hospitali ya Muhimbili, akiendelea kupatiwa matibabu kufuatia tukio la kupigwa risasi na aliyekuwa mchumba wake alfajiri ya huko maeneo ya Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambaye sasa ni marehemu. 
Kamanda Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa eneo la Hospitali ya Muhimbili mchana alipofika kujua kinachoendelea juu ya tukio hilo na maendeleo ya mgonjwa. 
Baadhi ya waandishi wa habari waliofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kumuona, lakini haikuwezekana kuruhusiwa kutokana na mgonjwa huyo.
Baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Redio One na ITV, wakiwa Hospitalini hapo wakisubiri kumuona mgonjwa.
Pia waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti walikuwapo hospitalini hapo.
 Baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Redio One na ITV, wakiwa Hospitalini hapo wakisubiri kumuona mgonjwa.
  Baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Redio One na ITV, wakiwa Hospitalini hapo wakisubiri kumuona mgonjwa.
 Wengine walianza kukata tamaa wakianza kutawanyika angalau kutafuta chochote.
Wapigapicha nao kwakisubiri kunasa picha ya mgonjwa huyo wakati akitolewa katika chumba cha Dharura.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UPDATE KUHUSU HALI MWANDISHI WA HABARI WA ITV UFOO SARO SIMULIZI ZA TUKIO LILIVYOKUWA
UPDATE KUHUSU HALI MWANDISHI WA HABARI WA ITV UFOO SARO SIMULIZI ZA TUKIO LILIVYOKUWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg11SL1ZUS_50GJI2HeZ7VG_pEfVH4ZEHjyZRfzv2KcvJTrIe8DodqTAYwRklVu09WG0Xv4kaoQcwuhQAQpGJSeOY7nPGSRzjCiHUf8h0QdXGoD5GmANj9N2pOHO1cgCHBlTiai25JsIdE/s640/UF3.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg11SL1ZUS_50GJI2HeZ7VG_pEfVH4ZEHjyZRfzv2KcvJTrIe8DodqTAYwRklVu09WG0Xv4kaoQcwuhQAQpGJSeOY7nPGSRzjCiHUf8h0QdXGoD5GmANj9N2pOHO1cgCHBlTiai25JsIdE/s72-c/UF3.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2013/10/update-kuhusu-hali-mwadishi-wa-habari.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2013/10/update-kuhusu-hali-mwadishi-wa-habari.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy