JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA Tele: +255 026 2322761-5 Fax No. +255 026 2324218 E-mail : cna@bunge.go.tz ...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
| ||
Tele: +255 026 2322761-5
Fax No. +255 026 2324218
E-mail: cna@bunge.go.tz
|
Ofisi ya Bunge,
S.L.P. 941,
DODOMA.
|
TANZIA
MAREHEMU KASUKU SAMSON BILAGO
(02.02.1964 – 26.05.2018)
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma, Mhe. Kasuku Samson Bilago aliyefariki leo majira ya saa 9 alasiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mhe. Bilago alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 22 Mei, 2018 akitokea Hospitali ya DCMC iliyoko eneo la Ntyuka Jijini Dodoma alikokuwa amelazwa awali.
Mwili wa Marehemu Mhe. Bilago unatarajiwa kuagwa Bungeni Dodoma siku ya Jumatatu tarehe 28 Mei, 2018 na baadae kupelekwa Kankonko Mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi. Ofisi ya Bunge inaendelea kuratibu taratibu za mazishi kwa kushirikiana na familia ya Marehemu na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi.
Imetolewa na: Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
26 Mei, 2018.
COMMENTS