Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae akizungumza na waandishi wa habari AFISA Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan At...
Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae akizungumza na
waandishi wa habari
Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae ameiomba Serikali
kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kuijenga barabara ya
Bagamoyo, Makurunge hadi kuingia Hifadhini ili kuondoa kero kwa watalii
hasa nyakati za mvua.
Hayo ameyazungumza kwenye maonyesho ya sita ya biashara ya Kimataifa
yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga na kusema ubovu
wa barabara hiyo umekuwa kikwazo kwa wageni wengi.
Mbae alisema Hifadhi hiyo imekuwa ikipokea wageni wengi kutokea Jijini
Dar es salaam na nje ya nchi kupitia barabara hiyo huku miundombinu hiyo
ikiwa haiwezi kupitika kwa nyakati zote.
"Wageni wetu wamekuwa wakitumia barabara hiyo kufika katika hifadhi yetu
na tuna idadi kubwa ya wageni hofu yetu ubovu wa barabara unaweza
kukwamisha wageni na labda kupungua"Alisema Mbae.
Aidha alisema uwepo wa miundombinu mizuri utarahisisha kwa wananchi toka
Mikoa ya Tanga,Dar na Pwani kutembelea katika hifadhi hiyo na kujionea
vivutio vilivyopo kwa siku moja.
Alisema ipo haja kwa Serikali kuelekeza nguvu kwenye ujenzi wa barabara
hiyo ili kuirahisishia hifadhi hiyo kupokea wageni wengi kwa nyakati
zote na kuongeza pato la Taifa.
Hata hivyo alisema Hifadhi hiyo imeweka mfumo wa matumizi ya master card
visa card katika maswala ya ulipaji wa gharama za ulipaji ili kudhibiti
mapato yaingiayo kama aerikali inavyoagiza.
"Tunamfumo wa kieletronics kwenye maswala yetu ya malipo na hii
itatusaidia kupunguza vitendo vya kihalifu kwa wageni wetu kutokana
kutokutembea na fedha nyingi"Alisema Mbae (Habari kwa Hisani ya Blog
ya Kijamii ya Tanga Raha)
COMMENTS