NAIBU WAZIRI DKT. NDUGULILE AZINDUA BODI YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
HomeJamii

NAIBU WAZIRI DKT. NDUGULILE AZINDUA BODI YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YARIDHIA VIPAUMBELE 23 VYA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA 2018/2019
WANAHABARI WATAKIWA KUFANYA UTAFITI WA HABARI ZAO
WAUGUZI,WAKUNGA WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI SEHEMU ZAO ZA KAZI






Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason (wa pili kulia) Sheria na kanuni zake zinazosimamiwa na Mamlaka ikiwa ni ishara ya kuizindua rasmi Bodi hiyo. Wengine katika picha ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Otilia Gowele (mwenye koti jeupe) na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia).


Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akiongea wakati anazindua Bodi Tendaji ya kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Mkemia, Dar es Salaam. Kushoto (waliokaa) ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Esther Hellen Jason na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko.


Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambayo ilizinduliwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kutoka kushoto waliokaa) kwenye ofisi za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.


Mameneja na wakuu wa Vitengo wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka hiyo ambayo imezinduliwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile leo kwenye ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Otilia Gowele (aliyesimama) akiongea kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kutoa hotuba na kuzindua rasmi Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo kwenye Ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akiwa pamoja na Wajumbe wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Kaimu Katibu Mkuu (Afya), Dkt. Otilia Gowele (wa pili kutoka kushoto) na Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Bi. Tunu Temu( wa kwanza kushoto).


Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali (CGLA) imetakiwa kuandaa mkataba wa utoaji huduma ili kuepuka ucheleweshaji katika utoaji wa majibu kwa wananchi wanaohitaji huduma za mamlaka hiyo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe saba.
"Mamlaka hii ni nyeti sana kwa hiyo tunatakiwa kuwa na mkataba wa utoaji wa huduma ili mtu akileta sampuli zake hapa afahamu lini atapata majibu hivyo kujiondoa kuwa sehemu ya ucheleweshaji wa utoaji wa haki," alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha,Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa ni lazima kuwa na ithibati kutokana na umuhimu wa Mamlaka hiyo kwani imepewa jukumu la kisheria kusimama Mahakamani kutoa majibu sahihi juu ya uchunguzi fulani hivyo ni lazima apatikane mtu wa kusimamia ubora ili majibu yanayotolewa yawe yanaaminika na kuweza kutumika ndani na nje ya nchi.

Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa Mamlaka imepata sheria mpya, muundo mpya, uongozi mpya pamoja na bodi mpya, hivyo imepewa meno ya kisheria katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu pamoja na kutatua changamoto zilizopo.

Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko ameiomba Serikali kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo zikiwemo za upungufu wa watumishi 172 pamoja na kununua mitambo ya kisasa kwani mitambo iliyopo haiendani na hali halisi.
Vile vile amemuahidi Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ataendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali ikiwemo suala la kuhamia jijini Dodoma.
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Esther Hellen Jason amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua katika nafasi hiyo ambapo amesema bodi itafanya kazi kwa weledi na kujituma ili kufikia matarajio ya nchi kama yalivyopangwa.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NAIBU WAZIRI DKT. NDUGULILE AZINDUA BODI YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
NAIBU WAZIRI DKT. NDUGULILE AZINDUA BODI YA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnKzKRK_iHewg9zUc-bfyxQiLOSPhOumQHK5C7-B1oM6ox3Qa5FV7s_KjVZor2w8O4QcAecmGWfmqIxxxC62pN8YePci_AOHs9RiqwNdU8zgKCx1O71vsLfkwGjBiVr1kkxjHO1mLAjng/s640/DSC_0430.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnKzKRK_iHewg9zUc-bfyxQiLOSPhOumQHK5C7-B1oM6ox3Qa5FV7s_KjVZor2w8O4QcAecmGWfmqIxxxC62pN8YePci_AOHs9RiqwNdU8zgKCx1O71vsLfkwGjBiVr1kkxjHO1mLAjng/s72-c/DSC_0430.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/naibu-waziri-dkt-ndugulile-azindua-bodi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/naibu-waziri-dkt-ndugulile-azindua-bodi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy