AQRB YATAKIWA KUJITANGAZA - MAJALIWA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria makabidhiano ya mashine 10 za kufyatulia matofali zilizotolewa na Bodi ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), kabla ya kufungua semina ya 29 ya wataalam hao, Mkoani Dodoma. Wa (tatu kulia) ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.


HomeJamii

AQRB YATAKIWA KUJITANGAZA - MAJALIWA

AQRB YATAKIWA KUJITANGAZA - MAJALIWA Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezungumzia juu ya umuhimu wa ...

AQRB YATAKIWA KUJITANGAZA - MAJALIWA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezungumzia juu ya umuhimu wa Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), kutangaza huduma wanazotoa za ujenzi ili kuwawezesha wananchi kuelewa na kuzitumia huduma hizo na hivyo kuboresha Sekta ya Ujenzi hapa nchini.
Akifungua semina ya siku mbili ya maadhimisho ya ishirini na tisa ya elimu endelevu kwa Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi jijini Dodoma, Waziri Mkuu amewataka wataalam hao kujiendeleza kitaaluma ili watoe huduma bora zaidi zinazouwiana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
‘Ongezeni wigo wa huduma zenu ndani na nje ya nchi ili huduma za ujenzi bora wa makazi katika miji na majini ziwe endelevu na zenye gharama stahiki”, amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu ameisisitiza bodi ya AQRB kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi na mafunzo ya ujenzi ili kuongeza idadi ya wanataaluma wanaoweza kujiajiri na kuajiri watu wengine.
Aidha, amehimiza Wizara ya Ujenzi kushirikiana na Wizara ya Afya na Tamisemi katika ujenzi wa vituo vya afya vya kisasa katika mikoa na halmashauri mbalimbali nchini.
Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewataka AQRB kuhakikisha wataalam wake wanashiriki kikamilifu katika miradi mikubwa ya ujenzi inayotekelezwa nchini ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), bandari na barabara ili kuwajengea uwezo mkubwa katika taaluma yao.
Amesisitiza kwamba Wizara imeanza kuandaa viwango maalum vya ujenzi vitakavyotumika katika ujenzi hapa nchini ili kuhakikisha kunakuwa na ustawi katika sekta ya ujenzi na makazi nchini.
Amezungumzia umuhimu wa AQRB kupambana na rushwa, kupunguza ada za ushauri ili kuwezesha wananchi wa kawaida kutumia huduma za kitaalam kutoka kwa wataalam hao.
Bodi ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) iliyoko chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inajukumu la kuratibu na kusimamia ujenzi kwa kusajili wataalam na makampuni ya ujenzi, kukagua miradi ya ujenzi na kutoa mafunzo kwa vitendo kwa watalaam wa ujenzi hapa nchini ambapo zaidi ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi 1520 wamesajiliwa.

(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akimsikiliza mwanafunzi wa mwaka  wa 4 wa kozi ya Usanifu Majengo, Kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Mwita Mgaya, kuhusu ujenzi wa kisasa wa majengo wakati Waziri Mkuu huyo alipotembelea banda  la chuo hicho kabla ya kufungua semina ya 29 ya wataalam hao, Mkoani Dodoma, kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.



Wajumbe wa Semina ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani), wakati akifungua mkutano huo wa siku 2 uliowakutanisha wataalam kujadili Mustakabali wa Viwanda nchini na namna ya kutunza majengo ya kale mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akifungua semina ya 29 ya Bodi ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Mkoani Dodoma. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa AQRB, Profesa Ninatubu Lema na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Eng. Binilith Mahenge.



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi baada ya kufungua semina ya 29 ya wataalam hao, Mkoani Dodoma. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa. (Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AQRB YATAKIWA KUJITANGAZA - MAJALIWA
AQRB YATAKIWA KUJITANGAZA - MAJALIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjTF1D_FxawY9g5t8kT0E3eV7qBtYjpllRGi_eCG0fuOsjIs4FEHi5YsvqjNARku6zzdwLjFHBUVtsPs4PYSuTz19Kfl0gd4V4JtwiaMxNnq7KiGnZQnxBn0vWcFhz9I3KCkFfseoXize8/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjTF1D_FxawY9g5t8kT0E3eV7qBtYjpllRGi_eCG0fuOsjIs4FEHi5YsvqjNARku6zzdwLjFHBUVtsPs4PYSuTz19Kfl0gd4V4JtwiaMxNnq7KiGnZQnxBn0vWcFhz9I3KCkFfseoXize8/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/aqrb-yatakiwa-kujitangaza-majaliwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/aqrb-yatakiwa-kujitangaza-majaliwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy