Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa leo Aprili 20, 2018 wilayani Kisarawe Mkoani Pwani baada ya kufanya jaribio la kupora ...
Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa leo Aprili 20, 2018 wilayani Kisarawe Mkoani Pwani baada ya kufanya jaribio la kupora walipovamia katika makazi ya mhasibu wa vikoba. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Polisi walipopata taarifa wakawahi eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na kupelekea vifo vya majambazi hao wanne. Miongoni mwa vitu vilivyokamatwa ni pamoja na bunduki aina ya AK 47, pingu, redio ya mawasiliano, risasi 51, bastola magari mawili aina ya Toyota.
COMMENTS