WATAKA SHERIA YA WATIA MIMBA WANAFUNZI IONGEZWE MENO
Baadhi ya wadau wa Elimu Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mkutano huo.
HomeJamii

WATAKA SHERIA YA WATIA MIMBA WANAFUNZI IONGEZWE MENO

Na Amina Hezron,  Morogoro Wito umetolewa kwa serikali kuhakikisha wanawadhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaoba...


Na Amina Hezron,  Morogoro


Wito umetolewa kwa serikali kuhakikisha wanawadhibiti na kuwachukulia hatua za
kisheria wale wote watakaobainika wamebaka au kuwapa mimba wanafunzi wa shule
za Msingi na Sekondari nchini.


 Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa elimu wilaya ya mvomero mkoani Morogoro wakati wa mkutano ulioandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania TEN /MET ili kupeana mrejesho wa namna ya kukabiliana na changamoto za mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.



Katika mkutano huo wa wadau  wamebaini ushiriki wa karibu wa wazazi na watoto wao haupo kwa kiasi kikubwa jambo linaloelekea kuendelea kuwepo kwa changamoto hiyo.

Kwa upande wake afisa elimu wa wilaya hiyo Bi. Maajabu Nkamyemka amesema kwa wilaya ya mvomero takwimu zinaonesha hadi April 6 mwaka huu takribani mimba 90
zimebainika kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambapo miongoni mwa
hizo mimba 13 ni kutoka shule za msingi.

Aidha Bi. Nkamyemka amesema kuwa ni jukumu la wazazi na walimu kwa kushirikiana na wanafunzi kuhakikisha wanawafichua wale wote ambao ni wahusika bila kuwafumbia
macho ili sekta husika kupambana nao ili kutokomeza janga hilo.

"kwa kuwa binti akipewa ujauzito huwa tunahangaika tu na aliyempa ujauzito, na yule
mwenye ujauzito tunamuacha sasa bhas sasa kwa kuwa wazazi hawataki kuleta
ushirikiano tutamfungulia kesi mwanafunzi mwenye mimba pamoja na wazazi ili
wazaz wawachunge watoto wao ipasavyo "Alisema Nkamyemka.
Wadau hao wa elimu wakiwa ndani ya mkutano huo 
Naye mratibu elimu wa kata za mhonda na Kweuma bwn, Heriamini Mariki amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya mimba hasa kwa wanafunzi, wa sekondari jambo ambalo kwa kiasi kikubwa wazazi ndiyo chanzo cha tatizo hilo huku akitaja sababu
zinazochangia kuwa ni pamoja na uelewa finyu wa wazazi na wakati mwingine
umaskini kwa baadhi ya kaya nyingi wilayani humo.

 â€œSisi kama wadau wajibu wetu mkubwa ni kuwapatia elimu wazazi juu ya athari za kutokaa karibu na watoto wao na kuwa wawazi juu ya madhara ya kufanya ngono wakiwa na umri mdogo" alisema Mariki

Naye diwani wa kata ya mhonda Bw. Abdallah Hassani Khalifa ametoa rai kwa Serikali
kujenga hosteli kwa shule za kata ili kuondokana na tatizo la mimba za utotoni
linaloikumba nchi nzima kwa kiasi kikubwa, huku akiwataka wazazi na walimu
wanawapa  watoto wanafunzi ushirikiano wa kutosha na ulinzi kwani ndiyo haki pekee wanaotakiwa kuzipata ili kufanya vyema katika masomo yao.





Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WATAKA SHERIA YA WATIA MIMBA WANAFUNZI IONGEZWE MENO
WATAKA SHERIA YA WATIA MIMBA WANAFUNZI IONGEZWE MENO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi2clXjVRIzbCWTxARnSOXLEuq-W2Ag7KIYStjUGry0kY-r_p8y4piFBkp8ssIVbGHtVhDeNZXabdhQoXB1PpP9f-MK5rMcCoatvvs1GfsUBPgysIKzDf8ryMlFnxaFZhGSxiyuh1UTN4P_/s640/cfd4e621-94ef-48e8-a36f-0db280a9dac4.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi2clXjVRIzbCWTxARnSOXLEuq-W2Ag7KIYStjUGry0kY-r_p8y4piFBkp8ssIVbGHtVhDeNZXabdhQoXB1PpP9f-MK5rMcCoatvvs1GfsUBPgysIKzDf8ryMlFnxaFZhGSxiyuh1UTN4P_/s72-c/cfd4e621-94ef-48e8-a36f-0db280a9dac4.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/wataka-sheria-ya-watia-mimba-wanafunzi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/wataka-sheria-ya-watia-mimba-wanafunzi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy