WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI
Afisa wa Kodi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Maternus Mallya (kulia) akitoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa na inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.

HomeJamii

WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI

Na Veronica Kazimoto,  Geita, 11 Aprili, 2018. Wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Geita wamejitokeza kwa wingi kupata elimu ...

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAJUMBE WA KAMATI YA PILI YA UCHUNGUZI WA MADINI YALIYOMO KWENYE MCHANGA KUTOKA MIGODINI
TAMKO LA THBUB KULAANI WATU KUTEKWA
RAIS DKTMAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI YA TAKUKURU YA 2016/2016



Na Veronica Kazimoto, Geita,

11 Aprili, 2018.
Wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Geita wamejitokeza kwa wingi kupata elimu ya mlipakodi inayoambatana na usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) pamoja na kupatiwa makadirio ya kodi kwa wafanyabiashara mbalimbali.
Akizungumza baada ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wa Wilaya ya Bukombe na Mbogwe wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa, Afisa Kodi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Maternus Mallya amesema mwitikio wa wananchi ni mkubwa na unaridhisha.
"Nimefurahishwa sana na mwitikio wa wananchi wa Mkoa wa Geita kwasababu wengi wameonyesha kiu ya kupata elimu na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi na mpaka sasa takribani wafayabiashara 200 wamesajiliwa na kupatiwa namba hiyo pamoja na kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato," alisema Mallya.
Nae mfanyabiashara wa kuchomelea mageti wa Wilaya ya Bukombe, Mandela Alex amesema kuwa, amefurahishwa na ujio wa kampeni hii wilayani kwake  kwani biashara yake imetambulika na kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa kibiashara.
"Kwakweli mimi nimefurahi sana kupata namba hii ya TIN na sasa biashara yangu ni halali na imeingizwa kwenye mfumo rasmi wa kibiashara na nitalipa kodi kulingana na makadirio niliyopewa na watalaam wa TRA," Alisema Alex.
Kwa upande wake mfanyabiashara wa vinywaji wa Wilaya ya Mbogwe mkoani hapa Beatha Kalungula ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Wilaya hiyo ambao hawajapata elimu na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi wafanye hivyo ili waweze kuwa na uelewa kuhusu kodi mbalimbali na biashara zao ziweze kutambulika.
"Mimi nimenufaika sana na elimu iliyotolewa hapa lakini pia nimefurahi mno kupata TIN namba ambayo itaniwezesha hata kupata mikopo kwenye taasisi mbalimbali za kibenki ambazo moja ya vigezo ni kuwa na TIN namba ya biashara yako, hivyo nawaambia wafanyabiashara wenzangu ambao hawajafika hapa, waje wakutane na wahusika wa TRA kwajili ya kupata elimu ya kodi  na kujisajili kama mimi nilivyofanya," alifafanua Beatha.
Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi mkoani Geita itamalizika tarehe 13 Aprili, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine, wafanyabiashara wapya wanasajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) pamoja na kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kodi na manufaa yake kwa Taifa.

Afisa wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) George Haule (kushoto) akitoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa na inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.





Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI
WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI
https://apis.mail.yahoo.com/ws/v3/mailboxes/@.id==VjN-DAAGW23ZtIGAxsZUlRBTluXZYsq1HNGkna5HdINtFs2Wi91KFN2mUvaQA8t8dQaAUWhjIv2uHVC2R0Wv8Q9VgQ/messages/@.id==AObWyQoAAAMTWs3-ZA8HqKSmIk4/content/parts/@.id==5/thumbnail?appId=YMailNorrin
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/wananchi-mkoani-geita-wajitokeza-kwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/wananchi-mkoani-geita-wajitokeza-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy