WANAFUNZI WA TANZANIA VINARA UANDISHI WA INSHA EAC NA SADC

Na Mwandishi Wetu Wanafunzi wa shule za Sekondari hapa nchini wameibuka washindi wa Tuzo za uandishi wa Insha zinazotolewa na Jumuiya ya...



Na Mwandishi Wetu

Wanafunzi wa shule za Sekondari hapa nchini wameibuka washindi wa Tuzo za uandishi wa Insha zinazotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC).

Akiongea mbele ya Wazazi na Walimu wa Wanafunzi waliopata ushindi wa insha hizo kwa  mwaka 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Wazara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu amesema washindi wa Tuzo hizo wametoa taswira tofauti na dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa elimu ya Tanzania si bora katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za kusini mwa Afrika.
Akifafanua Dkt. Semakafu amesema kuwa mashindano hayo ni kielelezo kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutoa elimu bora na wanafunzi walioshinda tuzo za uandishi bora wa insha wameonyesha kwa vitendo mafanikio ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta ya elimu.
‘’Matokeo ya Insha hizi pia yanaonesha picha tofauti na mawazo yaliyojengeka katika jamii kuwa shule binafsi ni bora kuliko shule za Serikali kwani baadhi ya wanafunzi kutoka shule za serikali wamejitokeza na kufanya vizuri katika mashindano ya uandishi wa insha.’’ Alisisitiza Dkt. Semakafu.
Mwanafunzi bora wa mashindano ya insha hizi kwa Jumuiya ya EAC ni Michael Msafiri  kutoka shule ya Sekondari Kibaha ya Mkoani Pwani.
Kwa upande wake Kaimu mratibu wa mashindano ya insha kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini mwa Afrika (SADC) Bw. Salum Salum amesema kuwa ushiriki wa wanafunzi katika uandishi wa insha umepanua maarifa ya wanafunzi walioshiriki katika shindano hilo.
“Maarifa ya wanafunzi yameongezeka hasa kuhusu mipango ya Jumuiya hizi na katika mchakato mzima wa mtangamano ndani ya Jumiya hizo na baina ya Jumuiya na Jumuiya” Alisisitiza Salum
Akifafanua amesema kuwa anawapongeza viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Mafunzo ya Amali Zanzibar na Baraza la Mitihani Tanzania kwa kusaidia kufanikisha mashindano hayo.
Pia alitoa wito kwa wakuu wa shule kuwasaidia wanafunzi kufuata taratibu zote za uandishi wa Insha kwa ufanisi ili kupanua wigo wa wanafunzi kushiriki katika mashindano hayo.

Hafla ya kuwatunuku tuzo washindi wa uandishi wa Insha hizo imefanyika leo mjini Dodoma ikihusisha Insha za Jumuiya ya Afrika Mashariki na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bi. Ave Maria Semakafu akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako  wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya Insha kwa washindi wa kitaifa kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), hafla hiyo  imefanyika leo mjini Dodoma .



Afisa Elimu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. James Njowi akitoa maelezo kuhusu mashindano ya mashindano ya Insha kwa washindi wa kitaifa kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), hafla hiyo  imefanyika leo mjini Dodoma.


Kaimu mratibu wa mashindano ya insha kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Salum Salum akitoa maelezo mafupi kuhusu mafanikio ya mashindano hayo leo mjini Dodoma wakati wa hafla yakuwatunuku zawadi kwa washindi wa shindano hilo.



Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Kagemuya  ya Mkoani Kagera Bw. Arnold Matungwa akipokea zawadi kama mmoja wa washindi wa insha hiyo wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi  hao leo mjini Dodoma.



Mshindi wa jumla wa insha kwa wa nafunzi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki Bw.   Michael Msafiri kutoka shule ya Sekondari Kibaha ya Mkoani Pwani.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bi Ave Maria Semakafu  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa insha kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), hafla hiyo imefanyika leo mjini Dodoma. (Picha zote na WEST)







COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANAFUNZI WA TANZANIA VINARA UANDISHI WA INSHA EAC NA SADC
WANAFUNZI WA TANZANIA VINARA UANDISHI WA INSHA EAC NA SADC
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1nPns9Wj-esiINAfMZpsf7FwRLoRqkpVkH6YNE8NE-9B3r1p-SordgpFmVWA6EDHpZ2XO2xwAWFLkk7xf-ByO5Aha15u4PxbbikDPdM0vElpKlpBdQdQmsmWqHOdxIShdvWF4hIICALA/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1nPns9Wj-esiINAfMZpsf7FwRLoRqkpVkH6YNE8NE-9B3r1p-SordgpFmVWA6EDHpZ2XO2xwAWFLkk7xf-ByO5Aha15u4PxbbikDPdM0vElpKlpBdQdQmsmWqHOdxIShdvWF4hIICALA/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/wanafunzi-wa-tanzania-vinara-uandishi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/wanafunzi-wa-tanzania-vinara-uandishi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy