OPERESHENI LIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KABLA YA TAREHE 30 APRILI KUEPUKA KUPELEKWA MAHAKAMANI YARINDIMA KANDA YA KASKAZINI
Wananchi wakisikiliza elimu ya kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati kutoka timu ya Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Halmashauri na Ofisi ya Kanda ya Ardhi ya Kaskazini katika eneo la Kilombero, Jijini Arusha.

HomeJamii

OPERESHENI LIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KABLA YA TAREHE 30 APRILI KUEPUKA KUPELEKWA MAHAKAMANI YARINDIMA KANDA YA KASKAZINI

Na Mboza Lwandiko Hivi karibuni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi alitoa nafasi ya upendeleo ya ongez...

EU INJECTS TZS. 1.4 BILLION TO COUNTER CHILD MARRIAGE AND FGM
DAWASCO YASHAURIWA KUTOA HUDUMA KWA UWAZI
MISA TANZANIA YATANGAZA MATOKEO YA UTAFITI WAKE KWENYE OFISI ZA SERIKALI

Na Mboza Lwandiko
Hivi karibuni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi alitoa nafasi ya upendeleo ya ongezeko la miezi minne kwa wamiliki wa Ardhi ambao bado hawajalipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati; ambayo hulipiwa kwa mwaka mara moja kila mwaka wa Fedha, ambapo malipo  hayo kwa utaratibu wa kawaida hufanyika kati ya mwezi Julai hadi Desemba kwa mwaka mpya wa Fedha, na hivyo kuanzia mwezi Januari Kodi ya pango la ardhi hutozwa pamoja na tozo /faini ya 1% kwa kila mwezi.
Mhe. Lukuvi alieleza utaratibu wa kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa mwaka  mpaka Desemba 30 na kuwa katika mwaka wa fedha huu 2017/18 ametoa ongezeko la muda wa kufanya malipo hayo na hivyo wamiliki wote ambao bado hawajafanya malipo hayo wafanye kwa kipindi hicho na kutoa tahadhari. Alisema; “ Ifikapo tarehe  30 mwezi wa nne nataka wananchi wote wanaomiliki Ardhi, kwa nyaraka za Hati na Offer wawe wameshalipa Kodi ya Pango la Ardhi yao kwa mwaka 2017/2018, endapo ikifika tarehe 30 Aprili hujalipa, kwanza; Tutawapeleka Mahakamani wote bila kujali nafasi zao, majina yao, au nafasi yoyote waliyonayo katika Taifa, Pili;  Tutawatangaza kwenye Magazeti ya Serikali ili wajue wanafisadi uchumi wa Taifa. Tatu; Upo uwezekano wa kufuta Viwanja au Mashamba mnayomiliki na Nne, upo uwezekano pia wa kuuza ardhi yoyote unayoimiliki ya nyumba au shamba ili Serikali iweze kufidia Kodi yake ya Ardhi”.
Mhe. Lukuvi alisema ili Mmiliki wa Ardhi aepukane na adha hiyo, Mmiliki husika wa Ardhi atapaswa kulipia Kodi ya Pango la Ardhi kabla ya tarehe 30 Aprili.
Dhana ya Ulipaji wa kodi ya Pango la Ardhi inatokana na Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 katika fungu la 3 kifungu kidogo cha 1(a).  Ambapo Kodi hukokotolewa kwa kuzingatia vigezo vikuu vitatu; Eneo kiwanja kilipo, Matumizi ya kiwanja yaliyoruhusiwa kwa mujibu wa hati miliki na Thamani na ukubwa wa kiwanja na madhara ya kutolipa Kodi ya Pango la Ardhi yameainishwa katika  sheria hiyo, fungu la 50 .
Pamoja na rai iliyotolewa na Mhe. Lukuvi ya kuzingatia kulipa Kodi ya pango la Ardhi kwa wakati kuepuka kupelekwa Mahakamani. Pia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha imeboresha Malipo ya ukusanyaji wa Kodi ya pango la Ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.
Serikali imeboresha mfumo huu wa ukusanyaji wa maduhuli kuwa wa kielektroniki, ili kurahisisha ukusanyaji wake na kuongeza uwazi miongoni mwa Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali.
Ulipaji Kodi ya Pango la Ardhi kwa njia ya simu ya mkononi  umeanza na kuendelea kutumika vyema Wizara ya Ardhi kwa Makusanyo ya pango la ardhi, ambao unamrahisishia mwananchi kulipia popote alipo kwa kutumia Tovuti ya Wizara au Simu Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kupatiwa hati  ataweza kutumia simu yake ya mkononi kuona kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Aidha, Mwananchi kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi kwa kutumia simu ya mkononi, Mwananchi anatakiwa kubonyeza *152*00# au kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi halafu anatuma kwenda namba 15200, baada ya hapo anaweza kulipia kwa njia ya Mpesa na Tigopesa au kulipia tawi lolote la Benki za NMB na CRDB.
Huduma nyingine za sekta ya ardhi, ambazo zinahusisha malipo haya ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi, kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official search), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya Ardhi zilizopo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia kwa njia ya benki na simu ya mkononi.
Kwa mmiliki wa Ardhi iliyopimwa na kupatiwa Hati ya umiliki, anaweza kuulizia kiasi cha fedha anayodaiwa na kulipia kodi ya Pango la Ardhi kwa kutumia Simu au Tovuti ya Wizara au kulipia Benki
Akizungumza na waandishi wa habari katika kuutambulisha mfumo wa GePG; Mkurugenzi wa Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano; Dkt. Shaaban Pazi alibainisha kuwa mfumo wa GePG, ulianza kutumika rasmi mwezi Juni mwaka jana katika Wizara ya Ardhi. Alisema; “Mafunzo ya awali yalitolewa kwa ofisi ya Dar es Salaam na kutolewa katika maeneo mengine. Alieleza kuwa Mfumo ni rafiki na utaboresha na kurahisisha ukusanyaji wa Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi.
Naye,  Mkurugenzi  wa Mifumo ya kifedha Wizara ya fedha; John Sausi amesema kuwa njia ya ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa mtandao utaiongezea Serikali kupata makusanyo ya ulipaji wa Kodi kwa wakati kutokana na makusanyo hayo kwenda moja kwa moja kwenye akaunti ya Serikali na kwamba utaondoa msongamano wa watu uliotokana na utaratibu wa awali wa Ulipaji Kodi.  Alisema Uanzishwaji wa mfumo huo utaenda sambamba na utoaji elimu ya jinsi ya kutumia kwa Wanachi waliokuwepo katika eneo la Wizara ili waweze kujihudumia kwa haraka na kwa uhakika.
Mwananchi; Halima Chitemi akiwa amepanga foleni ya kufanya malipo ya Kodi ya pango la Ardhi Wizarani, baada ya zoezi la utoaji wa elimu kufanyika kwake hakuwa tayari kuanza kufanya malipo hayo kwa njia ya simu akihofia kutofanikiwa kukamilisha malipo hayo. Hatahivyo, Bwn. Adam Manase ambaye alikuwa kwenye foleni hiyo hiyo nyuma ya Bi Chitemi alikubali kufanya malipo hayo kwa njia ya simu yake na kufanikiwa kufanya malipo yake vyema na kumuacha Bi Chitemi akisubiri kuhudumiwa kwenye foleni.
Mkuu wa Kitengo cha Kodi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dennis Masami amewahamasisha Wananchi kutambua sasa taratibu za ulipaji Kodi za pango la Ardhi zimebadilika, badala ya watu kufika Wizarani kwa ajili ya kufanya malipo ya Kodi ya pango la Ardhi, sasa wamiliki wa ardhi wafanye malipo hayo kwa nija ya kielektroniki.
Alisema; “Kwanza mtu ataweza kufanya makadirio ya kipi anadaiwa kwa njia ya simu au kupitia Tovuti Kuu ya nchi kufanya Makadirio, halafu kulipia kwa njia ya mpesa, tigopesa au benki husika”, ambayo ni njia rahisi zaidi kwao ambayo haitachukua muda wao mwingi”, alisema Masami.
Bwn. Masami alieleza ingawa Mfumo wa Kielektroniki  pia umerahisisha ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi na kuwezesha malipo kufanyika kwa ubora zaidi katika kuzuia mianya ya utapeli, changamoto kadhaa zimejitokeza ambazo Wizara imezibaini na inaendelea kuzifanyia kazi. Alisema changamoto kuu ni kuwa bado kuna kundi ambalo halina uwezo wa kufanya malipo hayo kwa kutokuwa na simu na huduma ya mtandao..
Bwn. Masami aliendelea kueleza; “Wananchi wengi ambao hawajapimiwa bado Ardhi yao, wamekuwa wakiuliza kuwa wao wanafanyaje malipo hayo? Hatahivyo, Wizara inaandaa utaratibu wa kusajili vipande vyote vya Ardhi ili Wamiliki wote wa Ardhi ya Mijini wahusike kulipa Kodi ya Pango la Ardhi”.
Pia kumekuwa na kundi la wamiliki wa ardhi kadhaa wanaofanya malipo hayo kielektroniki na kuhitaji risiti za karatasi (hard copy) zaidi ya zile zinazopatikanika kwenye simu, kuona usumbufu wa kupatikanika kwa risiti hizo, kwani huwalazimu bado kufika kwenye ofisi ya Halmashauri husika katika maeneo yao kupata risiti hizo.
Vile vile, Bwn. Masami aliongeza kusema kwamba;“Ujenzi wa mfumo wa kielektroniki wa kumbukumbu za Ardhi (Integrated Land Management System) ambao unaendelea kutekelezwa, ukikamilika utaboresha zaidi uwekaji wa kumbukumbu za wamiliki wa ardhi na hivyo kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Ardhi kwa ubora zaidi”. (Na Mboza Lwandiko – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi)



Ofisa Mwandamizi wa Ardhi kutoka Kanda ya Kaskazini; Bwn. Thadeus Riziki akitoa Elimu ya ulipaji wa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati katika eneo la Sakina kwa Iddi, Jijini Arusha. (Na Mboza Lwandiko – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: OPERESHENI LIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KABLA YA TAREHE 30 APRILI KUEPUKA KUPELEKWA MAHAKAMANI YARINDIMA KANDA YA KASKAZINI
OPERESHENI LIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KABLA YA TAREHE 30 APRILI KUEPUKA KUPELEKWA MAHAKAMANI YARINDIMA KANDA YA KASKAZINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhiIaerrSPDsxiFIYDt2-u1KttlbxJTEFvbpP1___pWfwaKfNCKqogRj90Wa8PP7B7piLUEbD3Bb1sFUNQIJlDptixi9R0px-e6_VEvylzR7jXqGQwCq1oQl9tSQD890a9n6ME0fF_St6E/s640/PIC+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhiIaerrSPDsxiFIYDt2-u1KttlbxJTEFvbpP1___pWfwaKfNCKqogRj90Wa8PP7B7piLUEbD3Bb1sFUNQIJlDptixi9R0px-e6_VEvylzR7jXqGQwCq1oQl9tSQD890a9n6ME0fF_St6E/s72-c/PIC+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/operesheni-lipa-kodi-ya-pango-la-ardhi_26.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/operesheni-lipa-kodi-ya-pango-la-ardhi_26.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy