Rais wa Uganda, Yoweri Museveni (mwenye mpama), "akikata kiu" kwenye nyumba moja, wakati wa ziara yake...
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni (mwenye
mpama), "akikata kiu" kwenye nyumba moja, wakati wa ziara yake ya
nyumbakwa nyumba kuhamasisha wananchi kuondokana na umasikini kupitia
operesheni aliyoanzisha ya "Vumbua Utajiri".
RAIS wa Uganda,
Yoweri Kaguta Museveni, ameanza kampenio ya nyumba kwa nhyumba aliyoipa jina la
“Vumbua utajiri” ikiwa na lengo la kuhamasisha umma kuondokana na umasikinikwa
kutumia mazingira yanayowazunguka.
Ili kuthibitisha
kuwa yeye ndiye anaanza na wengine wanafuata kwenye operesheni hiyo ya “Wealth
creation), Rais Museveni alichapisha picha kadhaa kwenye ukurasa wake wa
Facebook Oktoba 31, 2016 akiwa kwenye Kawaumu wilaya ya Luweero, ambapo
alionekana akikokota baiskeli iliyokuwa na dumu, akitoka kuchota maji ili
akamwagilie shamba lake la kahawa na ndizi.
Katika maneno
yake aliyochapisha kwenye ukurasahuo Rais alisema “Leo ni sikuya tatau ya
operesheni yangu ya Uvumbuzi wa utajiri hapa Luweero, Asubuhi hii nimechota
maji na kuyabeba kwenye baskeli yangu kwa nia ya kuonyesha umwagiliaji kwenye
shamba la Kahawa na Migomba ambayo nimepanda kwenye ekari 24 hivi karibuni nilizopewa
na serikali hapa Luweero. Nitaendelea na kampeni yangu ya mlango kwa mlango
kuhamasisha na kusisitiza juu ya operesheni “Vumbua Utajiri.”Alisema Rais
Museveni kwenye ukurasa huo wa Facebook.
COMMENTS