MWILI wa Marehemu Agness Gerald maarufu kama Masogange, utaagwa Aprili 23, 2018 kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Kwa...
MWILI wa Marehemu Agness Gerald maarufu kama Masogange, utaagwa Aprili 23, 2018 kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mratibu wa mazishi hayo, Steve Nyerere, baada ya shughuli ya kuagwa, mwili wa marehemu Masogange ambaye alikuwa video queen, utasafirishwa kwenda kwao mkoani Songwe kwa mazishi.
Kwa mujibu wa Nyerere Marehemu Masogange alifariki Aprili 21, 2018 majira ya saa 10 jioni wakati akipatiwa matibabu hospitali ya kibinafsi ya mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam.
“Marehemu alilazwa kwenye hospitali hiyo kwa siku nne akisumbuliwa na maradhi ya pumu, na ilipofika jana (Aprili 21, 2018), hali yake ilibadilika na kupoteza maisha.” Alisema Nyerere, mara baada ya kikao cha maandalizi ya mazishi kilichofanyika Leaders Club.
Kwa mujibu wa Nyerere, marehemu ameacha mtoto mmoja wa kike mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka 7.

MSANII Agnes Gerald a.k.a Masogange, (pichani juu), amefariki leo Aprili 20, 2018 wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya kibinafsi ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Taarifa zinasema, Masogange ambaye alikuwa “video queen” na umaarufu wake ulianza kuenea baada ya kuonekana kwenye video ya wimbo wa Masogange, uliotungwa na kuimbwa na msanii kutoka Morogoro Belle Nine, alifariki majira ya mchana baada ya kukimbizwa hospitalini hapo kwa matibabu.
Taarifa zaidi zinasema mwili wa Masogange ulihamishwa kutoka hospitalini hapo na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo msema ji wa hospitali hiyo, Aminieli Aligaisha amethibitisha hospitali hiyo kupokea mwili wa Masogange.
COMMENTS