MAZINGIRA YA UWEKEZAJI SEKTA YA FEDHA VIJIJINI KUBORESHWA
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji. 
HomeJamii

MAZINGIRA YA UWEKEZAJI SEKTA YA FEDHA VIJIJINI KUBORESHWA

Na WFM Serikali imeahidi kuboresha miundombinu na fursa nyingi za kiuchumi  katika maeneo ya vijijini ili kuweka mazingira bora na sa...

MDAHALO WAKUWANIA UONGOZI WA URAIS JUMUIYA YA WATANZANIA DMV
WAZIRI DKT. ATEUWA KALEMANI WAHANDISI 7 WATEULIWA KUSIMAMIA REAIII
TRA YATAMBUA UMUHIMU WA WAANDISHI WA MTANDAO KATIKA KUFIKISHA ELIMU KWA MLIPA KODI


Na WFM

Serikali imeahidi kuboresha miundombinu na fursa nyingi za kiuchumi  katika maeneo ya vijijini ili kuweka mazingira bora na salama yatakayovutia wawekezaji  katika sekta mbalimbali  hususani Sekta ya Fedha.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kalenga (CCM) Mhe. Godfrey Mgimwa aliyetaka kujua tamko la Serikali juu ya idadi kubwa ya benki za biashara kufunguliwa kwenye miji mikubwa.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa  miji mikubwa inakidhi vigezo muhimu vya uwekezaji kwa Sekta ya Fedha kama vile uwepo wa fursa nyingi za kiuchumi, miundombinu ya kisasa na usalama ikilinganishwa na maeneo ya vijijini.

Alisema kuwa kufuatia mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi nchini unaotekelezwa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990, shughuli nyingi za kiuchumi hususani benki zinaendeshwa na Sekta Binafsi .

“Kwakuwa Sekta Binafsi lengo lake ni kufanya biashara na kupata faida, uwanzishaji wa huduma za kibenki hutegemea upembuzi yakinifu ambao unazingatia fursa za kiuchumi zilizopo katika eneo husika, uwepo wa miundombinu wezeshi na usalama”, alisema  Dkt. Kijaji.

Alifafanua kuwa Serikali inachokifanya ni kuweka mazingira bora yatakayowavutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza maeneo ya vijijini kwa kuwa lengo ni kufikisha  huduma za kifedha kwa watanzania wote.

Katika swali la nyongeza la Mbunge huyo, alitaka kujua mbinu mbadala ya Serikali kuhakikisha inapeleka huduma za benki vijijini, kwa kuwa mpaka sasa Serikali bado haijaunda Sera ya kuhakikisha huduma hizo zinawafikia walengwa hasa wa vijijini.

Dkt.  Kijaji alieleza kuwa mpango mbadala wa kuhakikisha huduma za kibenki zinafika vijijini upo na Serikali inausimamia vizuri, na kuongeza kuwa mpango huo umeiwezesha Tanzania kuongoza katika huduma za fedha jumuishi barani Afrika.

Aidha Dkt. Kijaji alifafanua kuwa uwepo wa mawakala wa benki, kutolewa kwa huduma za kibenki kupitia Kampuni za simu ni ishara tosha kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha huduma hizo zinawafikia wananchi wote.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAZINGIRA YA UWEKEZAJI SEKTA YA FEDHA VIJIJINI KUBORESHWA
MAZINGIRA YA UWEKEZAJI SEKTA YA FEDHA VIJIJINI KUBORESHWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEgu-FtSDyw9WIobTMynaw0MtoeHKrBCPtViFSGqbX_5EMahggBTBQdRIQAGjV34tA1Dd1hEBtNDZz9tGBgiale3QpkrSAnTQ36aGIghVE6sHONu9hwVh0a0vTMiKsi0GXyNqRnCjiBxvsUI6zeoMdpNbQSldGoepufe1s_hWfp1w0Dc5A=s0-d
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEgu-FtSDyw9WIobTMynaw0MtoeHKrBCPtViFSGqbX_5EMahggBTBQdRIQAGjV34tA1Dd1hEBtNDZz9tGBgiale3QpkrSAnTQ36aGIghVE6sHONu9hwVh0a0vTMiKsi0GXyNqRnCjiBxvsUI6zeoMdpNbQSldGoepufe1s_hWfp1w0Dc5A=s72-c-d
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mazingira-ya-uwekezaji-sekta-ya-fedha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mazingira-ya-uwekezaji-sekta-ya-fedha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy