Tarehe 12 Aprili, 2018 Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alifanya ziara katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasin...
Tarehe 12 Aprili, 2018 Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alifanya ziara katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kukagua shughuli zinazotekelezwa na kituo hicho pamoja na kutatua changamoto mbalimbali. Katika ziara hiyo Mhandisi Luoga aliambatana na Kamishna Msaidizi wa Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya, wataalam kutoka Idara ya Nishati na mwakilishi kutoka Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).
Kamishna Luoga alielekeza kituo hicho kuendelea kuimarisha ulinzi ili kudhibiti upotevu wa mafuta. Aidha alielekeza kituo hicho kuendelea kushirikiana na wadau wengine kwa karibu zaidi katika kuboresha shughuli zake.
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (katikati) akielekeza jambo katika sehemu ya kupokea mafuta aina ya petroli na dizeli katika kituo hicho.
|
Sehemu ya gati za kupokea mafuta katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
|
COMMENTS