WAAJIRI WANAWAJIBIKA KISHERIA KUFANYA TATHMINI YA MAJANGA (RISK ASSESSMENT) MAHALAPA KAZI KILA MWAKA-WCF
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi,(WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja iliyowaleta pamoja mameneja na maafisa waajiri jijini Mwanza ili kupata elimu juu ya umuhimu wa kuzingatia kanuni za Usalama na afya mahala pa kazi ili kumlinda mfanyakazi na madhara yatokanayo na mazingira duni ya kufanyia kazi. Semina hiyo imefanyika jijini humo leo Machi 27, 2018 na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza. Katikati ni Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, ambaye idara yake ndiyo imeandaa semina hiyo.
HomeJamii

WAAJIRI WANAWAJIBIKA KISHERIA KUFANYA TATHMINI YA MAJANGA (RISK ASSESSMENT) MAHALAPA KAZI KILA MWAKA-WCF

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi,(WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, kwa niaba ya Mkurugenzi Mku...

WITO WA WADAU WA KUJA KUTOA MAONI KUHUSU MISWADA MITATU YA SHERIA
JNIA TBIII KUANZA KUTUMIKLA DESEMBA 2018 MHE. MBARAWA
SPIKA NDUGAI AKUTANA NA UMOJA WA WANAMICHEZO WA MPIRA WA MIGUU KUTOKA FC GRACE UNITED STATES OFISINI KWAKE MJINI DODOMA LEO





NA K-VIS BLOG/KHALFAN
SAID-MWANZA
TATHMINI ya majanga (risk assessment), mahala pa kazi inapaswa kufanywa
kila mwaka kwa mujibu wa sheria,
Meneja Tathmini za Usala na
Afya mahala pa kazi wa Mfuko wa
Fidia
Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Naanjela Msangi amesema.
Bi.
Msangi ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu tathmini ya majanga (Risk
Assessment) kwenye viwanda na maofisini wakati wa semina ya mafunzo kwa
Mameneja na Maafisa Waajiri waandamizi kutoka sekta ya umma na binafsi jijini
Mwanza, Machi 27, 2018.
“Sheria
inatamka kiwanda au ofisi yoyote ile inapaswa kufanya tathmini kabla ya kuanza
uzalishaji, majanga haya yanaweza kutokea wakati tayari uko kwenye operations,(uendeshaji) sasa ni vema uanze kufanya risk assessment kabla ya kuanza uzalishaji.”
Alifafanua.
Akizungumzia
sababu za kufanya tathmini kila mwaka, Meneja huyo alisema, yawezekana kiwanda au
ofisi kubadilisha njia ya uzalishaji kutoka ilivyokuwa awali hivyo
itasaidia kujua vile viwango vya hatari ya kutokea majanga vimeongezeka au la
ili uchukue hatua za kujikinga na kutokea kwa majanga mahala pa kazi.
Akifungua semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi
wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt.
Abdulsalaam Omar, aliwaasa waajiri kuzingatia sheria na mahusiano mahala pa
kazi ambayo pamoja na mambo mengine inamtaka mwajiri kuhakikisha wafanyakazi
wake wanafanya kazi katika mazingira salama, kwa kuwapatia vifaa vya kujikinga
na majanga (Personal Protective equipments).
“Pamoja
na wajibu wetu wa msingi wa kusajili waajiri na kuhakikisha wanawasilisha
michango ya kila mwezi kwa ajili ya wafanyakazi wao, ili panapotokea ajali,
kuumia au kifo mahala pa kazi na hatimaye Mfuko kuchukua jukumu la kulipa Fidia
kwa muathirika au wategemezi wake,
lakini pia tunalojukumu la kuzuia majanga yasitokee mahala pa kazi kwa
kutoa elimu na ndiyo lengo mahsusi la semina hii ya leo.” Alisema Dkt. Omar.
Alisema,
dhumuni lingine la semina hiyo ni kuzungumzia masuala muhimu kuhusu Mfuko
kupitia mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wataalamu wa WCF na masuala hayo
n I pamoja na kuhamasisha na kusisitiza wafanyakazi kuzingatia kanuni za kulinda
na kudumisha usalama na afya mahala pa kazi na masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi
wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.
“Vile
vile ni kuelimisha haki na wajibu wa mwajiri na mwajiriwa katika kuwezesha
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kushughulikia kwa ufanisi madai ya Fidia kwa
Wafanyakazi.” Alifafanua.
Kwa
ufupi niseme tu kwamba Mfuko una faida kubwa kwa Wafanyakazi, Waajiri na Taifa
kwa ujumla kwani hivi sasa wafanyakazi wanauhakika wa kinga ya kipato kutokana
na majanga yasababishwayo na ajali, magonjwa au vifo kutokana na kazi, alisema Dkt.
Omar.
Mmmoja
wa washiriki wa semina hiyo Bi.Asmini Gombo, ambaye ni Meneja Rasilimali watu wa kampuni ya
Mincom Rockdrills Tanzania Limited, alisema wao kama kampuni swala la kufanya
tathmini ya majanga mahala pa kazi lina umuhimu mkubwa kwani sio tu
linakusaidia kutambua ni vitu gani ambavyo kampuni inaweza kuboresha ili kuepuka
majanga lakini pia inasaidia kudumisha usalama na afya za wafanyakazi, “Sisi huwa tunafanya tathmini kila baada ya miezi mitatu na hii
imekuwa ikitusaidia sana kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu unazingatiwa na nitoe rai tu kwa wenzangu wajenge ratiba ya kufanya zoezi hili si lazima iwe kila baada ya miezi mitatu kama tunavyofanya sisi lakini hata kila baada ya miezi sita kwani utapunguza
majanga na hivyo kuokoa rasilimali watu na mali za kampuni pia." Alisema.


Pia alisipongeza WCF kwa kutoa elimu kwani awali walijua kazi kubwa ya Mfuko ni kusajili na kukusanya michango kutoka kwa waajiri kumbe pia inao wajibu wa kuelimisha waajiri kuepukana na majanga yanayoweza kutokea sehemu za kazi.

Asmini Gombo, Meneja Rasilimali watu wa kampuni
ya Mincom Rockdrills Tanzania Limited, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu elimu aliyopata kutokana na semina hiyo.


Washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Dkt. Omar.


Washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa semina.
Mshiriki akisoma kijarida chenye maelezo yahusuyo shughuli za Mfuko.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kushoto), Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia), na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine, wakiwa tayari kuanza kwa se mina hiyo.
Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. George Faustine, akitoa mada juu ya wajibu wa mwajiri kutekeleza sharia iliyoanzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi. ambapo alizungumzia wajibu wa mwajiri kujnisajili na Mfuko, kupeleka michango kila mwezi, na kutoa taarifa za wafanyakazi wake kwa usahihi.
Washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Dkt. Omar.







Washiriki kwa umakini wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa WCF.
Bi. Naanjela Msangi

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa WCF jijini Mwanza Machi 27, 2018.
Dkt. Abdulsalaam(kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki mwishoni mwa semina.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura Kunenge, (katikati), na Robert Duguza, (kushoto), Afisa wa usalama na afya mahala pa kazi wa Mfuko huo, wakimsikiliza mmoja wa washiriki ambaye alihitaji ufafanuzi Zaidi kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo Mfuko huo mwishoni mwa semina.
Meneja Tathmini za Usala na Afya mahala pa kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi(kushoto), akimsikiliza mmoja wa washiriki aliyehitaji ufafanuazi Zaidi wa masuala yaliyozungumzwa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar (mwenye tai) na Meneja Tathmini za Usala na Afya mahala pa kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi (wapili kulia), wakisikiliza hoja mbalimbali za washiriki wa semina mara baada ya kumalizika kwake.
Afisa Matekelezo (Compliance Officer), wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. George Faustine(mwenye tai), akifafanua masuala mbalimbali kwa washiriki mwishoni mwa semina hiyo.
Sehemu ya picha ya pamoja ya washiriki
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAAJIRI WANAWAJIBIKA KISHERIA KUFANYA TATHMINI YA MAJANGA (RISK ASSESSMENT) MAHALAPA KAZI KILA MWAKA-WCF
WAAJIRI WANAWAJIBIKA KISHERIA KUFANYA TATHMINI YA MAJANGA (RISK ASSESSMENT) MAHALAPA KAZI KILA MWAKA-WCF
https://i.ytimg.com/vi/Nqs23R3i4HA/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/Nqs23R3i4HA/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waajiri-wanawajibika-kisheria-kufanya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/waajiri-wanawajibika-kisheria-kufanya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy