WAZIRI KIGWANGALLA AITEMBELEA FAMILIA YA AKWILIN, ATOA UBANI KWA WAFIWA
HomeJamii

WAZIRI KIGWANGALLA AITEMBELEA FAMILIA YA AKWILIN, ATOA UBANI KWA WAFIWA

Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo ametembelea nyumban...


Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo ametembelea nyumbani kwa familia ya Akwilina na kutoa ubani wa pole kwa msiba huo.
"Nimefika hapa kama Raia mwema tu ambaye nimeguswa na msiba huu na nimetafakari kwani na mimi kipindi fulani nilipitia chuo hasa kutoka familia zetu hizi masikini kwa hiyo inapotokea ukio kama ili unaona ni pigo kwa familia, pigo kwa jamii, pigo kwa wanafunzi wenzake na pigo kwa Taifa kwa ujumla wake" alieleza Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na vyombo vya Habari msibani hapo.
Dkt. Kigwangalla ambaye alifika msibani hapo majira ya saa saba mchana, aliweza kuungana pamoja na ndugu na jamaa wa wafiwa ambapo pia alipata chakula cha mchana pamoja na waombolezaji wengine sambamba na kutoa ubani wake kama mwananchi mwingine.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli ambaye yupo hapo kwa ajili ya kusimamia shughuli  kwa upande wa Serikali, amebainisha kuwa wataendelea kuratibu baadhi ya mambo yanayoendelea hapo kwani msiba huo kwa namna moja Serikali imeguswa nao.
Mbali na Mkuu wa Wilaya hiyo, Wengine waliofika hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ubungo, John Kayombo ambapo kwa pamoja na watendaji wengine wa Kiserikali wameweza kusaidiana na familia ya marehemu katika shughuli mbalimbali zinazoendelea msibani hapo.
Aidha, jana viongozi wengine waandamizi wa Serikali akiwemo Waziri Elimu, Sayansi na Tekinolojia Mh. Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro waliweza kutembelea kutoa pole katika familia hiyo.
Akwilina kabla ya kifo chake alikuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya chama cha siasa cha CHADEMA. 
Marehemu Akwilina enzi za uhai wake
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa familia ya Akwilina alipotembelea hapo kutoa pole
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akipata taarifa kutoka kwa ndugu Akwilina amabye alikuwa ni mlezi wa binti huyo.
 
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakipata chakula cha mchana msibani hapo
Viongozi wa Serikali wakipata chakula msibani hapo
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya ndugu na jamaa walijitokeza katika msiba huo, Mbezi Luis, Jijini Dar e Salaam
  
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo.


Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makore akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI KIGWANGALLA AITEMBELEA FAMILIA YA AKWILIN, ATOA UBANI KWA WAFIWA
WAZIRI KIGWANGALLA AITEMBELEA FAMILIA YA AKWILIN, ATOA UBANI KWA WAFIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEj2l8lSj3dxvgtLPFyykzQldRH4q7iQsDJJA8s7r-KGFfcGKckP-O85lAh2ppLFe_J1i8_QRjeHqfWWkjrjHGOphuuiNqXzV4vF_r4yPRNG_Of7bhCh619hPtqo04ssWtVXdgwyWCjoCyGldJGc4P2tnGa_2UAfzvzY=s0-d-e1-ft
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEj2l8lSj3dxvgtLPFyykzQldRH4q7iQsDJJA8s7r-KGFfcGKckP-O85lAh2ppLFe_J1i8_QRjeHqfWWkjrjHGOphuuiNqXzV4vF_r4yPRNG_Of7bhCh619hPtqo04ssWtVXdgwyWCjoCyGldJGc4P2tnGa_2UAfzvzY=s72-c-d-e1-ft
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/waziri-kigwangalla-aitembelea-familia.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/waziri-kigwangalla-aitembelea-familia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy