UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI
HomeJamii

UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI

SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Kampuni ya Total wamekubaliana kuharakisha hatua zote za awali katika Mradi wa Bomba la...




SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Kampuni ya Total wamekubaliana kuharakisha hatua zote za awali katika Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga ili shughuli za ujenzi rasmi zianze mwezi Mei mwaka huu.


Makubaliano hayo yalifikiwa jana, wakati Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipokutana na uongozi wa juu wa kampuni hiyo wizarani mjini Dodoma.

Aidha, makubaliano mengine yaliyofikiwa katika kikao hicho ni kuwa, kazi za awali za maandalizi ya ujenzi ziwe zimekamilika ifikapo mwezi Machi mwaka huu.

"Ni lazima tuharakishe mchakato huu kama Mheshimiwa Rais Magufuli alivyoagiza. Hivyo, tumekubaliana kwamba shughuli zote za maandalizi ziwe zimekamilika ifikapo Machi mwaka huu ili kuwezesha shughuli rasmi za ujenzi wa Bomba kuanza mwezi Mei," alifafanua Waziri Kalemani.

Vilevile, katika kikao hicho, Rais wa Kampuni ya Total, Sehemu ya Afrika, Guy Maurice ambaye alikuwa kiongozi wa Ujumbe huo, alibainisha nia ya kampuni yake kuwekeza katika shughuli nyingine mbalimbali zinazohusiana na Mradi wa Bomba, jambo ambalo alisema litainufaisha zaidi Tanzania.

Mbali na makubaliano yote yaliyofikiwa, Waziri Kalemani pia alisisitiza kuwa ni muhimu kampuni ya Total iwasilishe Mpango-Kazi wake wizarani mapema iwezekanavyo ili utumike kama mwongozo-rejea katika kutathmini utekelezaji wa Mradi huo mkubwa.

Kampuni ya Total ndiyo mwekezaji katika utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi Lusius Mwenda, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Haji Janabi na maafisa wengine waandamizi kutoka wizarani.









Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI
UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwPketBuXe8vB9zXzNWJjtaDBpgQG9d9fm9OmaB_VPuupNMCN8x-QBxwMGWg8qTJJI7XpMiOak8uvtvdAH8IF5xpF4qwKPSL9GVcIvCVTtkKF_bqoTAQC848BZBdI_o6pJTy7UMsrqGUHE/s640/3.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwPketBuXe8vB9zXzNWJjtaDBpgQG9d9fm9OmaB_VPuupNMCN8x-QBxwMGWg8qTJJI7XpMiOak8uvtvdAH8IF5xpF4qwKPSL9GVcIvCVTtkKF_bqoTAQC848BZBdI_o6pJTy7UMsrqGUHE/s72-c/3.png
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/ujenzi-rasmi-bomba-la-mafuta-kuanza-mei.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/ujenzi-rasmi-bomba-la-mafuta-kuanza-mei.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy