SERIKALI YAIPONGEZA HOSPITALI YA HUBERT KAIRUKI KWA UJENZI WA JENGO LA KISASA KUSAIDIA WAJAWAZITO
HomeJamii

SERIKALI YAIPONGEZA HOSPITALI YA HUBERT KAIRUKI KWA UJENZI WA JENGO LA KISASA KUSAIDIA WAJAWAZITO

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange (kwanza) na  Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki ...

WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MUUNGANO
VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHIMIZA NIDHAMU-MAJALIWA
SADC ORGAN TROIKA MINISTERIAL ASSESSMENT FOLLOW UP MISSION



Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange (kwanza) na  Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki (wa pili)  wakiangalia ramani ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kinachotarajiwa kujengwa na Hospitali ya Hubert Kairuki hivi karibuni Bunju jijini Dar es Salaam. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG

Serikali imetoa pongeza kwa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki kupitia Hospitali ya Hubert Kairuki kwa kujipanga kujenga kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Ali Hapi kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo kitakachosaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999.

"Hatua Moja nzuri sana kwa manispaa yetu, maana huduma hii itapatikana hapa nchini jambo ambalo linaleta faraja sana kwa kuboresha huduma za afya kwa vile awali huduma kama hizo zilikuwa zikipatikana nje ya bara la Afrika... Mungu ni mwema itapatikana Tanzania," alisema Dkt. Dugange.

Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki alisema kuwa tatizo hilo lipo dunia nzima, na shirika la afya duniani lilitoa takwimu milioni 48 wanachangamoto ya kupata watoto.


Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki akielezea juu ya ujenzi wa kituo hicho cha kisasa.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Assey Mchomvu akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kujionea shughuli mbali mbali zilizokuwa zikiendeshwa na Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) kwa kipindi chote tokea Febriari 1-6, 2018 katika kuadhimisha Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999. Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone, Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki pamoja na mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange.
Wageni waliohudhuriwa sherehe hiyo.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange akipatiwa huduma za afya wakati aliposhiriki kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo kitakachosaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999.
Huduma za afya zikitolewa bure kwa wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.
Mpiga picha wa Gazeti la Nipashe, Mpochi akipatiwa huduma.

Mwandishi na mpiga picha wa Kajunason/MMG akipatiwa huduma.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YAIPONGEZA HOSPITALI YA HUBERT KAIRUKI KWA UJENZI WA JENGO LA KISASA KUSAIDIA WAJAWAZITO
SERIKALI YAIPONGEZA HOSPITALI YA HUBERT KAIRUKI KWA UJENZI WA JENGO LA KISASA KUSAIDIA WAJAWAZITO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVWUyS6EHV8IgL7X_9_cZTq8BWKokpP515eYqd0r6TaWTi3z-NXKV9WqHn-2wFSBN-eJZ3y0R8oTNt7P6zlF9tUGo3_MsOi-pc8Sgtj5g_l0zrWmwKXQEgi99FGsVMvBjK7K0zCRWsG5Y/s640/IMG_8158.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVWUyS6EHV8IgL7X_9_cZTq8BWKokpP515eYqd0r6TaWTi3z-NXKV9WqHn-2wFSBN-eJZ3y0R8oTNt7P6zlF9tUGo3_MsOi-pc8Sgtj5g_l0zrWmwKXQEgi99FGsVMvBjK7K0zCRWsG5Y/s72-c/IMG_8158.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/serikali-yaipongeza-hospitali-ya-hubert.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/serikali-yaipongeza-hospitali-ya-hubert.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy