BULYANHULU YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 75,649,524 KWA HALMASHAURI YA NYANG’HWALE
Meneja Mkuu wa Migodi wa  Bulyanhulu Benedict Busunzu akikabidhi hundi ya milioni 75,649,524  kwa Mkuu wa wilaya ya   Nyangh’hwale  Hamim Gweyama  kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya wilaya ya hiyo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba 2017.
HomeMikoani

BULYANHULU YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 75,649,524 KWA HALMASHAURI YA NYANG’HWALE

Meneja Mkuu wa Migodi wa  Bulyanhulu Benedict Busunzu akikabidhi hundi ya milioni  75,649,524   kwa Mkuu wa wilaya ya    Nyangh’hwale  Ha...




Meneja Mkuu wa Migodi  wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akizungumza na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale  ambapo alisema Acacia itaendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi .


Meneja Mkuu wa Migodi wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akifurahia pamoja na wafanyakazi wa Bulyanhulu baada ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale.








Na,Joel Maduka ,Nyang'hwale











Kampuni ya
uchimbaji madini ya dhahabu Acacia kupitia mgodi  wake  wa
Bulyanhulu imekabidhi hundi ya shilingi milioni  75,649,524 kwa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale
Mkoani Geita kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha Mwezi
Julai hadi Disemba mwaka 2017.


Akikabidhi
mfano wa hundi hiyo  mbele ya madiwani wa
halmashauri hiyo Meneja  wa  Mgodi
huo,  Benedict  Busunzu,
alisema  kawaida  mgodi
huo hutoa  ushuru  kwa  Wilaya  mbili
ya   Msalala  na
Nyangh’hwale  kwa  ajili
ya  miradi  ya
maendeleo.

Aidha  alitaja
moja  ya miradi  mingine
ambayo  mgodi  huo
umesaidia  Wilayani  humo
ni  pamoja  na
mradi  wa  mkubwa
wa  kusambaza   maji kwa
wakazi  150,000 wilayani  humo, 
wenye  gharama  ya
Shilingi  Bilioni 4.5  ambao
unatarajiwa  kukamilika  mwishoni
mwa  mwaka  huu.

Aidha kwa
upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Geita, Celestine Gesimba amewataka
madiwani    na watendaji  wa
halmashauri ya hiyo    kuepuka 
kutumia  fedha  zinazotolewa  na wadau
mbali mbali    kwa ajili  ya
miradi ya maendeleo  kwa  kulipana
posho  za  vikao, 
badala  yake  zote
zitumike  katika miradi  kwa
manufaa  ya  ustawi
wa wakazi  wa Wilaya  hiyo.

“Ninapenda  kuwaonya  viongozi
na watendaji    ambao mpo hapa Nyangh’wale  kuwa
tusitumie hizi  fedha  kwa
ajili  ya kulipana  posho
za  vikao  badala
yake  zote  zietumike
katika  miradi  ya
maendeleo  kwa  jinsi
mtakavyoainisha,”alisema Gesimba.

  Aidha Mkurugenzi  wa
Wilaya  ya  hiyo,
Carlos  Gwamagobe,  pamoja na kushukuru mgodi  mgodi
huo  kwa kuwapatia  fedha
hizo alisema ushuru wa huduma ambayo walikuwa wakipata hapo awali  umeshuka kwani kwa  kiasi kikubwa kwani walikuwa wakipokea
milioni mia nne kwa miezi sita .



“Tuna  imani
kuwa  mgodi  huu ukianza
shughuli  zake  kama
ilivyokuwa  awali   hata
ushuru  wa  huduma
utaongezeka  kwani awali  tulikuwa
tukipatiwa  kiasi  cha
Shilingi  Milioni  225 
lakini  tangu  kuibuka
kwa  sakata  la
Makinikia,  ushuru  nao
umepungua  mara  mbili
ya  zile  za
awali,”alisema Gwamagobe.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BULYANHULU YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 75,649,524 KWA HALMASHAURI YA NYANG’HWALE
BULYANHULU YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 75,649,524 KWA HALMASHAURI YA NYANG’HWALE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-JvbEsl9uq5_oiRYoRpQnDa62AIQk75_imvOg2fZXyDIz1S98RqiOlsc8bWKf6ri9w2cFD-HnxPCqBZx0ysE5yj5Qsb8My2K6sXqyWXHEgNbb5CxCMRTq7l7szqBZlVjznzD2oqBO6ZoQ/s640/DSC_1988.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-JvbEsl9uq5_oiRYoRpQnDa62AIQk75_imvOg2fZXyDIz1S98RqiOlsc8bWKf6ri9w2cFD-HnxPCqBZx0ysE5yj5Qsb8My2K6sXqyWXHEgNbb5CxCMRTq7l7szqBZlVjznzD2oqBO6ZoQ/s72-c/DSC_1988.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/bulyanhulu-yakabidhi-hundi-ya-shilingi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/bulyanhulu-yakabidhi-hundi-ya-shilingi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy