WAZIRI MKUU AAGIZA VIONGOZI NCHINI WATOE TAARIFA
HomeJamii

WAZIRI MKUU AAGIZA VIONGOZI NCHINI WATOE TAARIFA

*Ni kuanzia Mawaziri hadi Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wote, Naibu Mawaziri, M...

WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI INAKANUSHA TAARIFA ILIYOTOLEWA MKUTANO WA UONGOZI WA CHADEMA
MAKAMU WA RAIS AZINDUA MPANGO MKAKATI WA WATER AID TANZANIA
KAMATI YA MAKINIKIA YA TANZANIA YAANZA MAZUNGUMZO NA BARRICK GOLD CORPORATION JIJINI DAR ES SALAAM


*Ni kuanzia Mawaziri hadi Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wote, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Wakurugenzi watoe taarifa za fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi badala ya kusubiri ziara za viongozi wakuu.

Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Januari 6, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwenye kikao kilichofanyika hoteli ya Mt. Vicent, mjini Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.

“Kuanzia sasa ninaagiza, viongozi wote wa ngazi za juu wakiwemo Mawaziri hadi Wakurugenzi na hata ninyi wakuu wa idara mnawajibika kutoa taarifa za fedha tunazopeleka kwenye miradi kwa sababu wananchi wana haki ya kujua utekelezaji wa ahadi za Serikali,” alisema.

Alisema kila wanapoenda kwenye ziara ya kikazi vijijini, waelezee thamani za kazi zilizofanyika na waeleze ni lini miradi hiyo itakamilika.

“Mnapopata fursa ya kupanda jukwaani, tumieni wasaa huo kueleza kazi kubwa ambazo zimefanywa na Serikali. Elezeni Serikali imeleta fedha kiasi gani, kwa ajili ya kitu gani na kwa kufanya hivyo, mtasaidia kutoa taarifa za utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kampeni,” alisema.

Alisema wananchi wana haki ya kupatiwa taarifa za utendaji wa Serikali yao na akawataka viongozi hao wasisubiri ziara za viongozi wa kitaifa. “Nendeni mkaongee na wananchi, msiwaachie Wakuu wa Wilaya au Wabunge peke yao ndiyo waseme na wananchi,” alisema.

Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kukagua kituo cha kufua umeme kilichopo Unangwa, kuweka jiwe la msingi la ofisi ya TANESCO, kuzungumza na wananchi na kisha kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Songea.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAPILI, JANUARI 7, 2018.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AAGIZA VIONGOZI NCHINI WATOE TAARIFA
WAZIRI MKUU AAGIZA VIONGOZI NCHINI WATOE TAARIFA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJ2BhoyRaYOwqiIRYfO3fZ_m_J5S6QrV319wSVyz8ZRUnCA1oHB0dIrkGnjzYR1tv70DcoJgrkn-N6n2vX3XktaP3MhjAJY_eoyaLEa1wTu6xwCKMD6khcMRoudKUBgQbRl2VkEVBRTNVg/s320/WaziriMkuu.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJ2BhoyRaYOwqiIRYfO3fZ_m_J5S6QrV319wSVyz8ZRUnCA1oHB0dIrkGnjzYR1tv70DcoJgrkn-N6n2vX3XktaP3MhjAJY_eoyaLEa1wTu6xwCKMD6khcMRoudKUBgQbRl2VkEVBRTNVg/s72-c/WaziriMkuu.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/waziri-mkuu-aagiza-viongozi-nchini.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/waziri-mkuu-aagiza-viongozi-nchini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy