WAFURIKA OFISI YA RC MAKONDA KUDAI HAKI
HomeJamii

WAFURIKA OFISI YA RC MAKONDA KUDAI HAKI

ZAIDI ya Wananchi 3,000 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Januari 29, 2018 wamefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Sal...





ZAIDI ya Wananchi 3,000 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Januari 29, 2018 wamefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuitikia wito wa Mhe. Paul Makonda, kupeleka malalamiko ya kero zao zihusuzo dhulma walizofanyiwa.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, a,meandaa wanasheria 160, watakaopitia nyaraka mbalimbali zitakazowasilishwa na wananchi hao, ili kuwapatia ushauri wa kisheria.

Wananchi hao wametaabika kwa muda mrefu baada ya kudhulumiwa Mali zao Walizochuma kwa Tabu na sasa kupitia huduma ya Masada wa kisheria uliotangazwa na RC Makonda wanaamni watarejeshewa haki yao.

RC Makonda amesema idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza leo inatoa picha kamili Kuwa wapo viongozi wasiotekeleza vyema majukumu yao ya kiofisi kwenye idara zao ambapo ameahidi kuwawajibisha.

Aidha RC Makonda amesema kilichomgusa kuandaa Wiki ya msaada wa kisheria ni baada kubaini uwepo wa wananchi wanaonyanyasiki na hata kufikia hatua ya kufa kwa presha au kupooza miili baada ya kudhulumiwa na watu wenye pesa au wanaotumia uelewa wa sheria kukandamiza wanyonge.

Kutokana na idadi kuwa kubwa wanaoendelea kujitokeza RC Makonda anaongeza wanasheria wengi zaidi ili kuhakikisha Kila anaefika na kupata namba anahudumiwa ipasavyo ambapo amewaomba wanasheria kuhakikisha wanawasikiliza wananchi kwa umakini na kuchambua nyaraka kwa ufasaha na wasitoe hukumu.

Makonda amesema katika zoezi hili limehusisha Wanasheria wabobezi, Wataalamu wa kutambua nyaraka zilizogushiwa, watendaji wa Ardhi na watumishi wa Mahakama ambao wapo kwaajili ya kuwahudumia Wananchi.

RC Makonda amesema baada ya kupokea ripoti kamili ya kesi zote atasimama kuhakikisha Hakuna mnyonge anabaki akinyanyasika.

Zoezi la kusikiliza wananchi waliodhulumiwa Mali zao ikiwemo Nyumba, Viwanja, Magari, Mirathi na Kazi litaendelea hadi siku ya Ijumaa ya February 02.

Nao wananchi waliojitokeza wamemshukuru RC Makonda kwa kutambua Tabu wanazozipata baada ya kudhulumiwa na wajanja ambapo wengine wamesema wamepoteza Waume, Wake zao na wengine kupata magonjwa baada ya kudhulumiwa na wametaabika Muda mrefu kutafuta haki pasipo kufanikiwa lakini kupitia utendaji kazi makini wa RC Makonda wanaamni haki inapatikana.







Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAFURIKA OFISI YA RC MAKONDA KUDAI HAKI
WAFURIKA OFISI YA RC MAKONDA KUDAI HAKI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgY4MFe766gS-CejHxX9Xdu1iOhjRt6xoliY5OHd9ZteMhpcbk9bTuTNBuvBSyQBt3NtJW6K15cwKbdW3wyjZD3ImTr-04OjP2CcQbEVU6GaFylnNz8pYJFXv5flTEz725sMn_ybd6A0TxN/s640/MAK2.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgY4MFe766gS-CejHxX9Xdu1iOhjRt6xoliY5OHd9ZteMhpcbk9bTuTNBuvBSyQBt3NtJW6K15cwKbdW3wyjZD3ImTr-04OjP2CcQbEVU6GaFylnNz8pYJFXv5flTEz725sMn_ybd6A0TxN/s72-c/MAK2.png
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/wafurika-ofisi-ya-rc-makonda-kudai-haki.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/wafurika-ofisi-ya-rc-makonda-kudai-haki.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy