KAMATI YA RAIS YA KUCHUNGUZA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE YAANZA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA TANZANITE ONE
HomeJamii

KAMATI YA RAIS YA KUCHUNGUZA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE YAANZA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA TANZANITE ONE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz To...

NITAZINDUA KAMPENI YA KUPIMA VVU - WAZIRI MKUU
RAIS DKT. MAGUFULI AWAANDALIA FUTARI WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
RAIS DKT. MAGUFULI AWAANDALIA FUTARI WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite imeanza kufanya mazungumzo na kampuni ya Tanzanite One.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema mazungumzo hayo yaliyoanza tarehe 16 Januari, 2018 yanalenga kuhakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini hayo ambayo yanachimbwa nchini Tanzania pekee.
Prof. Kabudi amesema mazungumzo yameanza vizuri ambapo pande hizo mbili zinapitia matatizo yote yanayohusu biashara ya madini ya Tanzanite, utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za madini na mapato ya rasilimali hiyo, ili hatimaye zikubaliane namna bora itakayohakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanzanite One Bw. Faisal Juma Shahbhai amesema Tanzanite One ipo tayari kwa majadiliano hayo na inaunga mkono juhudi za kuhakikisha madini hayo yanainufaisha Tanzania tofauti na ilivyo sasa ambapo yanazinufaisha zaidi nchi nyingine ambazo hazizalishi Tanzanite.
Bw. Shahbhai ameongeza kuwa Tanzanite One itatoa taarifa zote zinazohitajika na wakati wote itatoa ushirikiano wenye lengo la kufanikisha mazungumzo hayo.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

17 Januari, 2018


Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana  jijini Dar es Salaam leo Januari 17, 2018 na wawakilishi wa kampuni ya Tanzanite One kabla ya kuanza na mazungumzo ambayo yanalenga kuhakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini hayo ambayo yanachimbwa nchini Tanzania pekee. (Picha na IKULU)



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMATI YA RAIS YA KUCHUNGUZA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE YAANZA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA TANZANITE ONE
KAMATI YA RAIS YA KUCHUNGUZA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE YAANZA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA TANZANITE ONE
https://lh5.googleusercontent.com/jbjg-KK-LZce4XrJB83y2aA5jitoaWYNsXoYjYRavBCc0D_yFQJdrW2mnF2oi_z4rCo58pT4i0KiGwCOsN2te3wOqwYyIhmeiGiyFQe7nRw1jQSPPj8Uw1aiHkunYoj4Sb_5Rtp_5OsF_ago6w
https://lh5.googleusercontent.com/jbjg-KK-LZce4XrJB83y2aA5jitoaWYNsXoYjYRavBCc0D_yFQJdrW2mnF2oi_z4rCo58pT4i0KiGwCOsN2te3wOqwYyIhmeiGiyFQe7nRw1jQSPPj8Uw1aiHkunYoj4Sb_5Rtp_5OsF_ago6w=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/01/kamati-ya-rais-ya-kuchunguza-biashara.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/kamati-ya-rais-ya-kuchunguza-biashara.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy