Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde akizungumza wakati wa semina kwa vijana kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupiti...
Dar es Salaam Jumapili 21 Januari 2018,
Takribani wanafunzi 10,000 tayari wameshajiandikisha na masomo ya ufundi ya VETA kupitia application ya VSOMO ili kusoma kozi mbalimbali za ufundi nchini. Mafunzo hayo ya ufundi ya VSOMO yanapatikana kupitia simu za mkononi kwa ushirikiano kati ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) yamekuwa nikichocheo kikubwa katika upatikanaji wa elimu kwa njia ya mtandao na kuongeza idadi ya wanafunzi wanataraji na wanaosoma masomo ya ufundi katika nyanja mbalimbali nchini.
Akiongea jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu program hiyo, Kaimu Mkuu wa chuo cha ufundi cha VETA kipawa, BwanaHarold Mganga alisema “ mafunzo ya ufundi ya muda mfupi yamekuwa yakitolewa na katika vyuo cha VETA kwa miaka mingi na hivyo idadi ya wanafunzi kuongezeka kila mwaka, kwa kuliona hilo VETA tukaona ni vyema kutanua wigo kwa kushirikiana na Airtel ili kutoa mafunzo haya kwa njia ya mtandao ili kuwawezesha vijana katika maeneo mbalimbali hususani maeneo ya pembezo au walio katika shughuli zao za kazi kupata nafasi ya kusoma masomo ya nadharia kupitia simu zao mahali popote wakati wotote kisha kufanya mafunzo ya vitendo katika vyuo vyetu vya VETA mara baada ya kafaulu mitihani yao. Najisikia fahari kusema kuwa ushirikiano wetu na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel umekuwa na tija kubwa katika kuwafikishia watanzania wote mafunzo haya kwa urahisi na ufanisi mahali popote nchini.
Mpaka sasa wanafunzi 9975 wamejiandikisha kupata mafunzo haya na Zaidi ya watanzania elfu 33 wameshapakuwa application ya VSOMO kupitia simu zao za mkononi. Kwetu sisi haya ni mafanikio makubwa na tuaamini kuwa mapinduzi haya ya elimu kupitia mtandao ndio yatakayoleta tija na kutuwezesha kuwa na nguvukazi yenye uledi ili kwenda sambamba na mahitaji ya nchi katika kufikia uchumi wa viwanda kwani nguvukazi ni moja kati ya nguzo muhimu katika kuendesha viwanda hivyo.
Kwa upande wake Meneja Mradi wa VSOMO Airtel, Bi Jane Matinde alisema “ Tunayo mikakati mingi mwaka huu itakayowezesha watanzania wengi hususani vijana kuvutiwa na kujiunga na masomo haya ikiwemo kuongeza idadi ya kozi, kutoa elimu kwa uma juu ya upatikanaji wamasomo haya, kuboresha namba yetu ya kituo cha simu cha VSOMO ya 0699859573 na0699859572 na masaa ya kupata huduma na vilevile kutanua wigo wa upatikanaji wa huduma hii na kuboresha malipo ya ada pamoja na mikakati mingi zaidi.
Lakini pia mkakati tulionao mpaka kufikia mwezi wa februari mwisho mwaka huu tutazindua kozi tano mpya ambazo ni pamoja na kozi ya usafi, kutengeneza Keki, kuoka mikate, ufugaji wa kuku pamoja na upambaji wamaua. Mpaka sasa tunazo kozi kumi na moja ambazo tayari tumeshazizindua na zinapatikana katika application hiyo ya VSOMO ambazo ni pamoja na kozi ya Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari, kutengeneza na kupamba keki, ufundi wa simu, ufundi pikipiki, Utaalamu saluni na urembo, ufuni wa kuchomelea pamoja na ufundi wa Aluminium..
Tunaamini upatikanaji wa kozi mbalimbali kutawezesha watanzania wengi kujiunga na kusoma masomo haya na kutanua wigo wa wanafunzi wengi zaidi kusoma na kupata vyeti kila mwaka. Tunatoa wito kwa vijana , wazazi na walezi kutumia mfumo huu kujiendeleza nakupata ujuzi zaidi aliongeza Matinde
Mpaka sasa mikoa minayoongeza kwa kuwa na mwitikio mkubwa wa wanafunzi kujiandikisha ni pamoja na Dar es saalam, Mwanza , Arusha, Morogoro na Dodoma huku vijana toka mikoa 26 nchini wamejiandikisha na mafunzo haya.
…………….mwisho………
Over 10,000 students register for VSOMO App
Dar es salaam Sunday 21 January 2018, Over 10,000 students countrywide have so far registered for Vocational Educational Training Authority – VETA through the VSOMO application in order to get vocational training of different courses. The VSOMO application is online learning which is being provided by VETA in partnership with Airtel Tanzania.
Speaking in Dar es Salaam over the weekend, the Kipawa VETA Deputy Principal Harold Mganga said that short vocational training has been being provided by VETA for quite long time now something which has attracted a large number of students. For that reason, VETA extended partnership with Airtel Tanzania to reach the growing number of students wishing to get enrolled to VETA and therefore introduced the e-learning through the VSOMO. ‘The application has been beneficial to students who cannot attend classes physically who those are fully engaged in other activities and would like to get vocational training. Through the VSOMO App, students get training through their smartphone mobile phones and only attend classes for practical’s and during examination period’, said Mganga.
So far, 9975 students have registered for the VSOMO App and over 33,000 have downloaded the App through their mobile phones. To us, this is a great success and we believe it brings the desired efforts needed to equip Tanzanians with different vocational training so that most of our youth can be able to employ themselves and also to bring a boost for country’s industrialization drive, added Mganga.
To her part, Airtel Tanzania VSOMO Project Manager Jane Matinde said that Airtel has put in place various initiatives for Tanzanians and especially the youth to benefit from the VSOMO App by adding courses. Matinde added that anyone wishing to join the project can call a free customer care numbers 0699859573 and 0699859572 from Monday to Friday.
VSOMO platform so far offers ten courses which are; includes electricity installation for domestic use, motorcycle mechanics, mobile phone repairs, aluminum production, welding, beauty care and modeling Catering and food services Techniques, PC maintenance, Industrial Electrical Installation, Domestic Plumbing, Auto –electrical and aluminum and Upvc Architectural Structure.
‘We are also looking to increase five new courses by February this year which are, office cleanliness, bakery, gardening keeping and chicken rearing’ added Matinde.
So the regions which have the highest number of VSOMO students are Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Morogoro and Dodoma.
COMMENTS