Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwa katika kituo cha Afya Ubwari wakati wa ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ...
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwa katika kituo cha Afya Ubwari wakati wa ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.
Aidha Jafo amewataka viongozi na watendaji kuendelea kushikamana ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Jengo la utawala na wagonjwa wa nje ya Hospitali ya Mvomero.
Jengo la utawala na wagonjwa wa nje ya Hospitali ya Mvomero.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametoa wiki sita kwa Mkandarasi wa mradi wa maji Kivindo Wilayani Muheza kukamilisha mradi huo na uanze kutoa huduma kwa wananchi.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake Wilayani Muheza ambapo alikagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Alisema Mradi huo kwas asa umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake na Mkandarasi umeahidi hapa mbele ya wananchi kwamba utaukamilisha ndani ya muda niliokupa ambao ni wiki sita kuanzia hivi sasa.
“Sitegemei kuskia sababu zozote zitakazofanya mradi huu usikamilike ndani ya wiki sita ni mategemeo yangu wananchi wataanza kufaidi matunda ya mradi huu baada ya muda mfupi tu kuanzia sasa, Mkandarasi fanya kazi yako” Alisema Jafo.
Katika ziara hiyo Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea Miradi ya afya na elimu katika kituo cha afya Mkuzi na Ubwari pamoja na kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kilulu.
Waziri Jafo amewapongeza wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Serikali katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Maeneo ya Umma. Hususan ni Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI) kwa kutoa mifuko 50 ya Saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Ubwari.
Halkadhalika Waziri Jafo ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha ajenda ya maendeleo kwa wananchi.
Tamisemi ya Wananchi.
COMMENTS